• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

"UVAAJI BARAKOA DAR ES SALAAM SASA SIO HIARI NI LAZIMA" RC MAKALLA

Posted on: July 26th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Amos Makalla akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mapema leo.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Mhe Amos Makalla ametoa tamko hilo leo ofisini kwake wakati anaongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mwongozo wa udhibiti wa ugonjwa wa “UVIKO -19” kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mhe Mkuu wa Mkoa amezitaka kamati zote za ulinzi na usalama katika wilaya za Mkoa  kusimamia katika maeneo yao utekelezaji wa mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto katika kukabiliana na wimbi la tatu la kuenea kwa ugonjwa wa KORONA au UVIKO-19.

“Kuanzia leo wananchi wavae barakoa katika maeneo mbalimbali iwe ni kwenye Daladala, Mwendokasi na vyombo vingine vya usafiri, aidha vyombo vya umma vya usafiri kuwe na “level seat” vilevile maeneo yote ya mikusanyiko iwe kwenye sherehe, matamasha, kwenye ibada na hata maofisini viwepo vifaa vya maji tiririka  na vitakasa mikono” Alisema RC Makalla

Sambamba na hilo Mhe Mkuu wa Mkoa amesema shughuli zote za kiuchumi katika Mkoa wa Dar es Salaam ziendelee kama kawaida lakini taadhari dhidi ya KORONA au UVIKO – 19 zichukuliwe tena kwa umakini mkubwa kwa kuwa ugonjwa huo upo nchini.

Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam imejipanga vizuri kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza katika kukabiliana na ugonjwa huo, tayari ofisi yake ilishafanya ziara katika vituo vya afya na Hospitali za Mkoa kujiridhisha uwepo wa vifaa vya kuweza kutoa huduma pale wagonjwa wakibainika.

Msisitizo wa mkuu wa Mkoa kwa wananchi wote ndani ya Mkoa ni kusitisha mikusnyiko isiyokuwa ya lazima, katika maeneo ya Stendi za mabasi, daladala, bodaboda kuzingatia ukaaji wa umbali wa zaidi ya mita moja kati ya mtu na mtu, kunawa maji tiririka, kutumia vitakasa mikono na uvaaji wa barakoa.

Mwisho jukumu la Mkoa sasa ni kufanya ziara za kushitukiza kutembelea maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es salaam kuona utekelezaji wa mwongozo huo wa udhibiti wa ugonjwa wa KORONA kupitia afua ya kudhibiti misongamano katika jamii bila kuathili shughuli za kiuchumi na ofisi ya Mkoa ipo tayari.

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA HABARI NA UHUSIANO

MKOA WA DAR ES SAALAM.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa