• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

" Usafi ni DSM ni Ajenda ya Kudumu" RC Chalamila.

Posted on: September 16th, 2023

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo Septemba 16, 2023 wakati wa maadhimisho ya siku ya usafi Duniani katika viwanja vya Zakhiem Mbagala Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.

RC Chalamila amekemea tabia za kuto zingatia taratibu za usafi kama vile mtu amepanda kwenye gari la Umma akula kitu baadae anatupa barabarani bila aibu pia kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi na hata madereva wa bodaboda wanavyopaki ovyo barabarani amesema kituo chochote kikiwa mahali pasipo sahihi ni Uchafu hivyo usafi ni pamoja na mtu kuwa katika eneo lake stahiki.

Aidha Mhe Chalamila amesema suala la usafi lazima liwe ajenda ya kudumu katika Wilaya zote za Mkoa huu, pawepo na mjadala mpana katika vikao mbalimbali vya Halmashauri vilevile  Usalama wa Mkoa ni ajenda za kudumu katika Mkoa zingine zinafuata " Taka ni Uchafu na Uchafu ni maradhi, tengenezeni By Laws za kudhibiti uchafu na jamii lazima itii sheria bila shuruti " Alisema RC Chalamila

Vilevile Mhe Mkuu wa Mkoa amesema Mhe *Selemani Jafo* alitakiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo kutokana na sababu zisizo zuilika ameshindwa kuja hivyo ameniagiza niwaambie yuko pamoja nanyi na anawashukuru kwa namna mnavyounga mkono utekelezaji wa majukumu yake katika wizara anayoiongoza, ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Rais Muungano na Mazingira.

Sambamba na hilo maadhimisho hayo yameongozwa na kauli mbiu "Tuungane Pamoja Kujifunza Kupanga na kuhimiza Uimarishaji Huduma za Udhibiti wa Taka" ambapo *Mhe Chalamila* ameshiriki kufanya usafi na kujionea maonyesho mbalimbali na namna ya kuthibiti taka ambayo yalikuwa yanaonyeshwa na wadau wa Mazingira katika viwanja hivyo na baadae kukabidhi tuzo kwa makundi mbalimbali ishara ya kutambua mchango wao katika usimamizi wa mazingira

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Mobhare Matinyi amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuendelea kusimamia usafi katika wilaya Temeke kwa  kufanya hivyo ni njia nzuri ya kuzuia magonjwa  milipuko na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Ifahamike kuwa maadhimisho ya siku ya usafi Duniani huadhimishwa kila jumamosi ya wiki ya tatu Septemba kila mwaka na kwa Tanzania mara ya kwanza maadhimisho hayo yalianza kuadhimishwa mwaka 2008

Matangazo

  • MWENENDO WA BEI WIKI YA 8-12 DESEMBA 2025 DSM December 08, 2025
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • MWENENDO WA BEI WIKI YA 1-5 DESEMBA 2025 December 01, 2025
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Ziara ya Naibu Waziri OWM-TAMISEMI MHE Reuben Kwagilwa Dar

    December 22, 2025
  • RC Chalamila Vyombo vya Habari ni Muhimili Muhimu kwa Taifa

    December 05, 2025
  • RC Chalamila Azindua Wodi ya Watoto Wachanga Hospitali ya Amana

    December 03, 2025
  • Rais Dkt Samia Suluhu Akutana na Wazee wa Dar es Salaam

    December 02, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa