• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

UJENZI WA OFISI ZA WALIMU DAR ES SALAAM SASA KUANZA RASMI

Posted on: September 19th, 2017


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo amezindua rasmi zoezi la ufyatuaji wa Matofali kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu ambapo amewasihi wadau na wananchi kuunga Mkono jitihada hizo.

Katika uzinduzi huo Mhe. Makonda ameshiriki zoezi la ufyatuaji wa Matofali kwa ajili ya Ujenzi huo.

Mhe. Makonda amesema lengo la Ujenzi wa Ofisi hizo ni kuboresha Mazingira ya kufanya kazi kwa walimu ili waweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi na kuongeza ufaulu.

Amesema wapo wengi waliopanga kufanya ujenzi wa Ofisi za Walimu lakini mipango hiyo iliishia kubaki kwenye makarabrasha maofisini lakini kupitia juhudi zake na Kamati aliyoiunda wameweza kuleta matokeo chanya.

RC Makonda ametoa wito kwa wananchi na wadau kuchangia mabati, saruji, kokoto, mchanga, nondo au nguvu kazi ili kuwawezesha walimu kufanyakazi katika mazingira bora.

Amesema hataki kuona kwenye Mkoa wake walimu  wanadhalilika kwa kukosa ofisi na vyoo hali inayopelekea kujisaidia kwa majirani, bar au vichakani.

Aidha amesema hadi sasa amefanikiwa kupata mifuko zaidi ya 10,000 ya saruji mashine za kufyatulia matofali, gurdoza na vifaa vingine ambapo ataendelea kugonga hodi kwa wadau ili waweze kuchangia ujenzi huo.

Amewaomba Wananchi kuwa na uzalendo kwa kujitoa katika ujenzi huo iwe kwa mtu binafsi au Vikundi vya Joaging, Timu za Mpira na vikundi vya maendeleo.

Ameipongeza Kamati ya ujenzi wa Ofisi za walimu, JKT, Jeshi la Magereza, Jeshi la Polisi, NHC, TBA, Channel Ten na Umoja wa Wamiliki wa Malori na wengine kwa namna wanavyojitoa kusaidia katika zoezi hilo.

Katika hatua nyingine RC Makonda amesema atatoa TV 30 kwa Magereza ya Ukonga, Segerea na Keko ili wafungwa wapate fursa za kutazama hotuba za Rais DR.JOHN MAGUFULI ili wajue maendeleo yanayofanyika uraiani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu Canal Charles Mbuge amesema hadi sasa kiasi cha fedha kilichotumika ni zaidi ya Million 200 ambapo watahakikisha ujenzi huo unakamilika.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa