• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Tope na Takataka Vyachangia Daraja la Jagwani Kuziba Nyakati za Mvua

Posted on: November 13th, 2023

Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa,  Waziri wa OR-TAMISENI Mhe. Mohamed  Mchengerwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Novemba 13, 2023 wamefika na kukagua athari za mvua katika daraja la Jangwani na kutoa kauli ya Serikali kuhusu hatua zinazofanyika sasa na zinazotarajiwa kufanyika ambazo ndio mwarobaini wa kuondoa kabisa kero zinazowakabili wananchi  hasa nyakati za mvua.

Viongozi hao waliwasili katika eneo hilo nakujionea hali ya daraja lilivyo ambapo wameona tope  na takataka zikiwa zimezagaa chini ya daraja hilo na kuleta adha kwa wanaotumia daraja hilo, maji kushindwa kupita na kusababisha mafuriko hali inayowapatia ugumu wenye vyombo vya moto na wapita kwa miguu.

RC Chalamila alisema, "Sisi kama mkoa tuna wajibu wa kuangalia jambo lakufanya kila siku ya Mungu, jambo moja wapo ni kuhakikisha tunaendelea na uzibuaji wa daraja hili ili maji yaendelee kupita kirahisi."

Aidha Mhe Chalamila amesma kuna ulazima wa kuongeza kina na kutoa elimu ya mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na elimu ya usafi wa mazingira kwa jamii kutokana na utupaji ovyo wa takaka na machupa zinazotokana na shughuli za kibinadamu hali inayopelekea kuziba kwa daraja hilo.

Pia Mhe Chalamila alitoa rai kwa wananchi wanaoishi mabondeni wahame, "Viwanja ni kweli walinunua wao, nyumba walijenga wao na kuhama tunaomba na tuwashauri kwamba chukueni jukumu la kuondoka kama mnadhani maji yanaweza kuleta athari ila kwa wale wabishi mimi sina kipingamizi, utaishi na maji sawa, lakini kama utakufa utaleta hasara kwa taifa na familia yako," alisema RC Chalamila.

Naye Waziri wa Ujenzi Mhe. Bashungwa amemtaka meneja wa TANROAD Mkoa kuhakikisha takataka na tope lililojaa eneo la daraja linitolewa ili maji yaweze kupitana sio kusambaa na kupita juu ya daraja sambamba na hilo kugusia pia juu ya ubunifu wa daraja kubwa litakalokuwa suluhu ya muda mrefu.

Vilevile Waziri wa TAMISENI Mhe. Mohamed Mchengerwa amehimiza na kuwataka wakuu wa Mikoa na Wilaya watoke maofisini na kwenda kuangalia hali wanazopitia wananchi wao hasa kipindi hiki cha mvua nyingi na watatue kero zao wasishie tu kukaa maofisini kusubiri kuletewa taarifa

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Temeke Yang'ara Mwenge wa Uhuru 2025

    June 02, 2025
  • RC Chalamila: Miradi 36 yenye Thamani ya Tsh 79,255,160,719.44 Kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Dar

    June 01, 2025
  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa