• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

SHOW ROOM ZA MAGARI ZOTE JIJINI SASA KUWA ENEO MOJA

Posted on: September 11th, 2017


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda ameanza kutekeleza AHADI aliyoitoa baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alipofanya mkutano na wenyeviti wa serikali za mitaa kuhusu Kupanga Mji katika muonekano mzuri wa jiji la biashara utakaovutia wananchi wengi wa ndani na nje kuja kufanya biashara Dar es Salaam kwa kuzindua mpango mkakati wa Ujenzi wa Eneo Moja kubwa la kufanyia biashara ya kuuza magari (used cars) pamoja na vifaa vya magari na huduma zingine zinazoendana na Biashara hiyo ikiwemo Utoaji wa bima na lesesni za magari, Huduma za kibenki, Ofisi za mamlaka ya Mapato (TRA) katika eneo moja (one car stop center) katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Mhe Paul Makonda amesema tayari Serikali ya Mkoa imeshatenga eneo kubwa na la kutosha katika Manisapaa ya Kigamboni ambalo litatumiwa na wafanyabiashara wote wa magari katika Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo katika utekekezaji wa mpango huo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda ametoa "OFFER" ya Bure kwa miaka mitatu kwa wafanyabiashara kutumia eneo hilo pasipo Malipo au tozo ya Kodi ya Pango au Kiwanja hatua itakayowawezesha kutumia unafuu huo kujenga uzio na Sehemu za Ofisi katika maeneo hayo, ambapo apo awali wafanyabiashara hao hulazimika kulipa zaidi ya Shilingi milioni Sita kwa ajili ya gharama za kupangisha eneo la kufanya biashara, ambapo kwa sasa watakaa Bure kwa Miezi 36 pasipo kulipa Gharama za Pango

Mhe Paul Makonda amesema azma ya serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam ni kutengeneza mazingira mazuri yatakayovutia wawekezaji kuwekeza ambapo katika hatua za awali tayari wafanyabiashara wameonyesha nia ya Kujenga (show room) kubwa za kuuzia magari ambazo zitatumika kuuza magari mpaka yatakayouzwa nje ya nchi, na ndani ya Tanzania.

Mkakati huu pia unalenga kudhibiti vitendo viovu na ukwepaji kodi unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara ya magari wasiowaaminifu ambapo katika mpango huu, mteja atapata fursa ya kufika kwenye eneo moja na kuchagua gari analotaka, na kisha kulipia fedha, na kodi ya serikali, na leseni, pamoja na Bima katika eneo moja hatua ambayo itaongeza ukusanyaji wa Mapato ya serikali na kudhibiti Madalali ambao wamekuwa wakipandisha gharama za uuzaji wa magari kwa maslahi yao binafsi.

Utaratibu huu utakuwa ni wa kwanza kuwahi kutekelezwa katika nchi za ukanda wa Africa mashariki, ambao unafanana na utaratibu wa kuuza Magari unaotumiwa katika majiji ya Tokyo Japan, na Dubai nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu ambapo kuanzia Leo tarehe 11/09/2017 maeneo yataanza kutolewa BURE kwa wafanyabiashara wote wenye Show room za Magari jijini na baada ya Miaka mitatu Wanaotaka kununua watanunua, na wanaotaka kuendelea kupangisha watapangisha, zoezi hili  litahitimishwa mwezi January 2018 ambapo anaamini Show room zote zinakuwa zimehamia Kigamboni, na hakutakiwa tena kuwa na uuzaji wa Magari kiholela katika Mkoa wa Dar es Salaam zaidi ya Kigamboni.

Mhe Makonda amehitimisha kwa kusema mpango huu unaendana na utekekezaji wa AGIZO la Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli la kuwataka Wakuu wa Mikoa kuainisha maeneo ya uwekezaji kwa wafanyabiashara wa ndani na nje yatakayovutia wananchi kuwekeza nakurahisisha utoaji wa huduma bora kwa Wananchi, na kusititiza kuwa Mpango huo utachochea ushindani halali wa biashara ya Magari, ushindani ambao mwisho wa siku utatoa huduma bora kwa Wananchi.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa