• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Serikali yaja na Mwarobaini wa Changamoto ya Kivuko Magogoni-Kigamboni

Posted on: January 23rd, 2025

 

-Yazindua vivuko 2 vya kisasa

-Kivuko kimoja kinauwezo wa kubeba watu 250 kwa mara moja kwa kasi ya dakika 5 hadi 6.

Waziri wa Ujenzi Mhe Abdallah Ulega leo Januari 23, 2025 amezindua mashirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi katika kituo cha Magogoni kwa kuzindua rasmi vivuko 2 ambavyo vitatoa huduma kwa wananchi, uwekezaji wa vivuko hivyo umefanywa na Azam Marine.

Akiongea wakati wa hafla hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, RC Chalamila amesema tumefika hapa mara kadhaa tumeona namna watanzania wenzetu wanavyohangaika kwa kuwa bado Serikali ilikuwa haijatoa majawabu sahihi ya changamoto za vivuko.

Hivyo amemshukuru Mhe Rais Dkt Samia kwa kutafuta suluhu ya kilio cha wana Ilala, Wanakigamboni na watanzania kwa ujumla ambapo leo inajidhihirisha kupitia uzindua vivuko hivyo 2 Sea Tax 3 na Sea Tax 4 pamoja na kuweka mfumo wa kidijitali wa kukatisha Risiti na Kituo cha Kisasa cha Abilia kusubiria vivuko "Huo ni uwekezaji unaojibu changamoto za wananchi naipongeza sana Azam Group niwaombe muendelee kuwekeza na maeneo mengine" Alisema RC Chalamila .

Aidha RC Chalamila amesema TANROAD wana maeneo ya hifadhi za barabara ambayo  ni vichaka, hivyo ameshauri maeneo hayo wapewe watu ambao wako serious na uwekezaji ambao utakuwa na tija na masilahi mapana kwa umma.

Sanjari na hilo vivuko hivyo vilivyozinfuliwa leo vinauwezo wa kubeba watu 240 kwa wakati mmoja kwa kasi ya dakika 5 hadi 6 hivyo uwekezaji huo unakwenda kuondoa kabisa changamoto ambayo wananchi wamekuwa wakiipata kwa kipindi kirefu.

Kwa upande wa Wakuu wa Wilaya ya Ilala na Kigamboni wamemshukuru Mhe Rais kwa juhudi zake na maono katika kuleta ustawi kwa jamii hapa nchini hususani Wilaya ya Ilala ,Kigamboni na Mkoa kwa ujumla.

Mwisho maboreho ya vivuko hivyo na uwekezaji wa vivuko vipya unaendelea sio tu Magogoni bali hata maeneo mengine kama ziwa Victoria, Tanganyika  na Ziwa Nyasa


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa