• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makonda: Wanaotumia watoto Yatima,Walemavu na Waishio Mazingira Magumu kama Kitega Uchumi Kukiona cha moto

Posted on: June 29th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametangaza vita na watu wenye tabia za kuwachukuwa watoto yatima,walemavu na waishio katika Maisha magumu Kama mitaji ya kujinufaisha watakamatwa na kuchukuliwa hatua Kali za kisheria.

RC Makonda ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya matokeo ya utafiti wa idadi ya Watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani kinyume na Sheria hali inayopelekea kushindwa kutumia fursa ya Elimu Bure iliyotolewa na Rais Dkt. John Magufuli jambo ambalo RC Makonda ameapa kulivalia njuga.

Utafiti huo umebaini Mkoa wa Dar es salaam pekee una jumla ya watoto 3,312 wanafanya kazi mitaani na kati ya hao watoto 2,984 walionekana wakifanya kazi nyakati za mchana na 328 wanafanya kazi nyakati za usiku.

RC Makonda amesema idadi hiyo ya watoto wanaoishi mitaani ni matokeo ya kukosekana kwa misingi bora ya familia na mmonyoko wa maadili ndio maana aliamua kuunda tume ya kupitia sheria ya mtoto na mikataba ya kimataifa ambayo itasaidia kuweka haki stahiki za watoto.

Aidha RC Makonda amewaonya watu wenye tabia ya kuwapatia ombaomba fedha barabarani kuwa Ndio wanaohalalisha uwepo wa watu hao ambapo amesema Kama mtu anataka kweli kusaidia waishio maisha magumu wapeleke misaada kwenye vituo vilivyopo kwa mujibu wa sheria kwakuwa vituo hivyo vinafuatilia mienendo ya watoto kitabia, elimu na matibabu ambapo ukimpa pesa mtoto barabarani unatengeneza mazingira ya kuwa na fedha ambayo hana uhalali nayo na anapokuwa mtu mzima anakuwa mkabaji,mporaji na kuchoma visu watu wasio na hatia.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la Babawatoto Center Bwana Mgunga Mwa Mnyenyelwa amempongeza RC Makonda kwa kufanya Zoezi la kutafuta haki ya mtoto alietelekezwa kwakuwa kupitia Zoezi hilo limewezesha watoto wengi kuingia kwenye mfumo rasmi wa kupata fedha ya matunzo kila mwezi pamoja na bima ya matibabu Bure.

Amesema utafiti huo umefanywa na shirika la Babawatoto Center for Children and Youth kupitia mradi wa USAID Kizazi Kipya kwenye mikoa mitano ambapo wamebaini nusu ya watoto wa mitaani wanapatikana mkoa wa Dar es salaam.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa