• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC MAKONDA AZINDUA RASMI UJENZI WA OFISI 402 ZA WALIMU DAR KWA KISHINDO

Posted on: November 1st, 2017


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA leo amezindua zoezi la ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema ujenzi wa Ofisi hizo utaenda kwa kasi ya hali ya juu chini ya Vijana wenye morali ya kazi kutoka JKT, Magereza na Jeshi la Polisi.

Ofisi hizo za kisasa zitakuwa na Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Mwalimu Mkuu Msaidizi, Ofisi ya Walimu wa kawaida, Mhasibu, Karani, Chumba cha kuhifadhi Mitihani, Vyoo vya kisasa, Stoo, Jiko, Chumba cha Mikutano na sehemu kuweka Mafaili ambapo ndani ya ofisi zitafungwa AC, Feni, Samani, Taa za kisasa na Umeme.

Akizungumza Katika uzinduzi huo ulioenda sambamba na upandaji wa Miti RC MAKONDA amesema kuwa lengo la ujenzi huo ni kuwezesha Walimu kufanyakazi katika Mazingira mazuri yatakayowapa morali na hamasa ya kufundisha Wanafunzi.

Aidha RC MAKONDA amesema kama Walimu wakiboreshewa Mazingira ya kufanya kazi itasaidia kukuza ufaulu.

RC MAKONDA amepongeza Walimu kwa kuwezesha Mkoa wa Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika mtihani wa Darasa la saba ikitokea nafasi ya nne mwaka jana na kuwahimiza kukamatia nafasi hiyohiyo.

"Rais MAGUFULI ameshatuonyesha dira kwa kutoa elimu bure na sisi wasaidizi wake ni lazima tuendeleze maono yake, mimi sio kiongozi wa kusubiri kuagizwa ndio nifanye kazi kama ilivyo kwa Remote hadi ibonyezwe ndio ifanye kazi, mimi ni kiongozi wa kujiongeza, sijachaguliwa kuwa mzigo kwa serikali bali kuleta matumaini kwa wananchi" Alisema RC MAKONDA.

Amewataka Viongozi kuacha Siasa kwenye mambo ya Msingi yanayolenga kuleta maendeleo kwa kuwa Maendeleo hayana chama wala ubaguzi wa Dini.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam LAZARO MAMBOSASA Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu, Maafisa Elimu, Wakuu wa Shule ambapo Wote kwa pamoja wamepongeza hatua ya RC MAKONDA kujenga ofisi za Walimu.


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Temeke Yang'ara Mwenge wa Uhuru 2025

    June 02, 2025
  • RC Chalamila: Miradi 36 yenye Thamani ya Tsh 79,255,160,719.44 Kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Dar

    June 01, 2025
  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa