• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makalla Tuna Mafuta ya Kutosha Kutumia Mpaka Julai 15,2022

Posted on: April 22nd, 2022

- Ni Mafuta yaliyopo Sasa na Yale yaliyopo kwenye Meli.

- Asema Hakuna uhaba wowote wa Mafuta nchini kwa mafuta ya Dizel, petrol, mafuta ya Taa Na Ndege.

- Ampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka Mpango mzuri uliowezesha Nchi kuwa na akiba ya kutosha.

- Atangaza matokeo ya kamati ya uchunguzi  juu ya wezi waliochepusha mafuta bomba kuu kuwa walikamatwa na wako mikononi mwa vyombo vya sheria.

- Bomba lipo Salama Baada ya kufukuliwa lote na kufukiwa upya, chombo Cha kufuatilia usalama wa bomba kinunuliwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema kiasi cha akiba ya nishati ya mafuta kilichopo Sasa na yale yaliyopo kwenye Meli yakishushwa yatatosha kutufikisha mpaka July 15 mwaka huu hivyo hakuna sababu yoyote ya Wananchi kuwa na hofu.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam alipokutana Na wadau wa mafuta Na wakala wa uagizaji mafuta pamoja kwa lengo la kutoa mrejesho wa kamati ya uchunguzi wa wizi wa mafuta Na kupokea taarifa ya hali ya mafuta nchini.

Aidha RC Makalla amesema kiasi Cha Mafuta yaliyopo Sasa ukijumlisha na Yale yatakayoshushwa na Meli yatafanya Nchi kuwa na akiba ya Lita Milioni 512.7 za Dizeli, Petrol Lita Milioni 365.5, Mafuta ya ndege Lita Milioni 40 na Mafuta ya taa Lita Milioni 5.9 ambapo kwa pamoja yanaweza kutumika mpaka July 15 mwaka huu.

Kutokana na Mkoa wa Dar es salaam kuwa lango kuu la Biashara ya mafuta, RC Makalla amesema Serikali itaendelea kulinda na kudhibiti Miundombinu ya Mafuta* ili kutokomeza tatizo la Wizi na uchepushaji wa Mafuta na usalama wa Wananchi ambapo amesema kwa Sasa Bomba la Mafuta lipo salama.

Hata hivyo RC Makalla ametoa Matokeo ya Kamati aliyounda kuchunguza Wizi wa Mafuta kutoka bomba kuu ambapo amesema zaidi ya watu 15 walikamatwa na wapo Chini ya Vyombo vya sheria na kueleza kuwa tayari Serikali imefanyia kazi mapendekezo ya Kamati ikiwa ni pamoja na kufukua upya Bomba la Mafuta na kulifukia na ununuzi wa kifaa Cha kutambua wapi Bomba limechepushwa.

Kuhusu suala la foleni za malori Bandarini zinazosababishwa na upanuzi wa Barabara, RC Makalla ameelekeza Shughuli za Ujenzi kufanyika pasipokuathiri Shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja Ujenzi  barabara ya kuingia Na kutoka bandarini kufanyika usiku.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wakala wa uagizaji Mafuta kwa pamoja Erasto Simon na Wadau wa Mafuta kwa pamoja wamemshukuru RC Makalla kwa hatua za haraka alizochukuwa kudhibiti tatizo la Wizi na uchepushaji wa Mafuta lililokuwa limedumu kwa muda mrefu na Sasa wanakiri kupokea kiasi Cha Mafuta sawa na kile walichoagiza

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa