• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makalla Apokea Mpango Kazi wa Machinga Mkoa wa DSM

Posted on: April 28th, 2022

 

- Wamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan Na  Serikali kuwajali Na kushirikishwa

- Waomba Mkoa usimamie uanzishwaji Saccos ya Machinga Mkoa

- Waahaidi kushirikiana Na TRA kudhibiti walipa kodi.

- RC Makalla awaahidi kuyafanyia kazi Mapendekezo yote ya SACCOS Na uboreshaji maeneo wanayofanyia biashara.

- RC Makalla athibitisha mapato yamepamda baada ya machinga kupangwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo April 28 amepokea Mpango kazi ulioandaliwa na Machinga wa Mkoa huo uliosheheni Maoni na mapendekezo ya kuwezesha ufanyaji Biashara kwa ufanisi mkubwa zaidi ili kuleta Matokeo chanya.

Miongoni mwa Mambo yaliyowasilishwa kwenye Mpango kazi huo ni pamoja na Udhibiti wa majanga ya Moto, Maboresho ya maeneo walipopelekwa Machinga, Kulindwa kwa maeneo waliyoondoka ili yasivamiwe upya, Udhibiti wa masoko yasiyo rasmi,  Uanzishwaji wa SACCOS ya Machinga, Ushirikiano kwenye udhibiti wa upotevu wa mapato, Uanzishwaji wa Machinga marathon kwaajili ya kuchangia Damu na Uwepo wa takwimu kamili ya idadi ya Machinga na kupatikana kwa ofisi ya Machinga.

Akizungumza wakati wa kikao Cha pamoja na Viongozi wa Machinga kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa, RC Makalla amepokea kwa mikono miwili ombi la Mkoa kusimamia Uanzishwaji wa SACCOS ya Machinga ambapo ameunda Kamati itakayojumuisha Wataalamu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wilaya na Viongozi wa machinga.

Aidha RC Makalla amesema miongoni mwa kazi ya Kamati itakuwa ni kufanya mapitio ya katiba, kuainisha sifa za mwanachama ili kujirudhisha.

Hata hivyo RC Makalla amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira walipohamishiwa Wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na kuanzisha route za Daladala kuchochea Biashara ambapo ameelekeza hata Fursa za mikopo zitolewe kwa waliopo kwenye maeneo waliyopangwa.

Pamoja na hayo RC Makalla amesema tangu zoezi la kuwapanga vizuri Wafanyabiashara waliokuwa wakifanya biashara holela lifanikiwe Mapato yamepanda kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es salaam Namoto Yusuph amemshukuru RC Makalla kwa kutenga muda wa kuwasikiliza ambapo wameomba Serikali iweke Mkazo kwenye suala la kuzuia na kudhibiti upotevu wa mapato kupitia udanganyifu unaofanywa na Wafanyabiashara kwenye mashine za EFD na risiti za kusindikiza mzigo ambapo risiti moja inaweza kutumika kwenye mizigo mingi zaidi.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa