• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makalla Atoa Maelekezo Matano Kwa Walimu Wakuu DSM

Posted on: January 11th, 2022

- Ataka Ongezeko la uandikishaji watoto Elimu ya Awali na Darasa la kwanza

-Asisitiza kutokana na uhaba wa Ardhi msimamo wa Mkoa ni kujenga Madarasa ya magorofa

- Akemea Uvamizi wa maeneo ya shule, awataka walimu Wakuu kuwasilisha taarifa za migogoro ya Ardhi katika maeneo yao

- Asema Ujenzi wa Madarasa umekamilika Walimu kwa umoja wao waunge Mkono Juhudi na ubunifu wa Rais Samia

- Awataka Walimu kushiriki kikamilifu katika Kampeni mbalimbali zinazofanyika katika Mkoa wa DSM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla ametoa maelekezo hayo leo Januari 11,2022 wakati wa kikao kazi na walimu wa Kuu wa shule za msingi na Sekondari DSM katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Shaban Robert, Ilala Jijini Dar es Salaam.

Aidha RC Makalla amepongeza kazi inayofanywa na walimu wote wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkoa umekuwa ukifanya vizuri Kitaaluma kupitia matokeo ya mitihani ya taifa lakini pia hata nyanja za michezo Mkoa umekuwa ukifanya vizuri.

Hata hivyo RC Makalla amesema takwimu za Uandikishaji hadi sasa Elimu Awali ni asilimia 39 na Darasa la kwanza ni asilimia 68 kwa hiyo kasi zaidi inahitajika ili watoto wote wennye sifa waandikishwe.

RC Makalla amekemea  michango mbalimbali isiyofuata taratibu ambayo ni kikwazo kwa wanafunzi wakati wa kujiandikisha ambapo amesisitiza watoto wasiziiliwe kwa sababu ya sweta, au mchango wowote.

Vilevile RC Makalla amesema msimamo wa Mkoa kwa sasa ni kutumia vizuri Ardhi kwa kujenga Madarasa ya magorofa kwa kuwa idadi ya wanafunzi imekuwa ikiongezeka kila siku wakati Ardhi ni ilele.

Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa amekemea Uvamizi wa maeneo ya shule na kuwataka Wakuu wa Shule kwa kushirikiana na Watendaji wa Kata na Mitaa kuwasilisha taarifa za migogoro ya Ardhi ili iweze kufanyiwa Kazi, na ameelekeza Wakurugenzi kupima maeneo ya shule.

RC Makalla amesema Ujenzi wa Madarasa umekamilika amewapongeza Walimu wakuu kwa kusimamia vizuri Ujenzi huo tena kwa Kipindi kifupi ambapo Mkoa wa Dar es Salaam umefanikiwa kujenga Madarasa 743 na bweni moja Walimu wana kila sababu ya Kuunga mkono ubunifu na Uzalendo wa Rais Samia Suluhu wa kutafsiri vema matumizi ya Mkopo wa Uviko 19.

Mhe Makalla amewataka Walimu kushiriki kikamilifu katika Kampeni mbalimbali zinazofanyika katika Mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DSM kwa kuhakikisha maeneo ya shule yanakuwa safi Vilevile Kampeni ya Kuwapanga vizuri wamachinga wahakikishe wanalinda maeneo ya shule yasivamiwe na wafanyabiashara wadogo.

Kwa Upande wa Afisa Elimu Mkoa Ndg Abdul Maulid akitoa takwimu ya Uandikishaji wa watoto Elimu Awali na Darasa la kwanza amesema kwa sasa takwimu zimeongezeka wiki iliyopita Uandikishaji Elimu Awali ulikuwa asilimia 32 na Darasa la kwanza asilimia 52 lakini hadi sasa takwimu zimeongezeka, Elimu Awali asilimia 39 na Darasa la kwanza asilimia 68


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa