- Amshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa wakati.
- Ujenzi umefikia Asilimia 40 na Mkandarasi yupo ndani ya Muda.
- Asema maandalizi ya Mpango wa Kariakoo kufanya Biashara saa 24 yanaendelea vizuri
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amemuelekeza Mkandarasi wa Kampuni ya Estim Construction Ltd kuongeza Kasi ya Ujenzi na Maboresho ya Soko la Kariakoo likamilike kwa wakati ili Nia njema ya Rais Samia Suluhu Hassan kuona Wafanyabiashara wa Kariakoo wanafanya biashara katika mazingira Bora inatimia.
RC Makalla amesema hayo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa Soko lililoungua na Soko jipya lenye urefu wa gorofa 6 ambapo Ujenzi unaghahirimu zaidi ya Shilingi Bilioni 26.
Katika Ziara hiyo RC Makalla ameonyesha kuridhishwa na Kasi ya Mkandarasi ambae mpaka Sasa amefikia Asilimia 40 jambo linloleta matumaini ya Soko kukamilika kwa wakati.
Aidha RC Makalla amemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa kwa wakati jambo linalomuwezesha Mkandarasi kutekeleza Majukumu yake pasipo usumbufu wowote.
Pamoja na hayo RC Makalla amesema kukamilika kwa Soko Hilo itabadili mfumo wa uendeshaji biashara kwa kutoa Wigo mpana wa kupokea Wafanyabiashara wengi Zaidi kutoka *Wafanyabiashara 600 mpaka kufikia Wafanyabiashara zaidi ya 2,000.
Kuhusu suala la Kariakoo kufanya biashara saa 24 Kama Rais Samia alivyoelekeza, RC Makalla amesema kikosi kazi kinaendelea kufanya tathimini Kisha kitawasilisha taarifa kwaajili ya utekelezaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa