• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makalla Apokea Ujumbe Kutoka Chuo Cha Ukamanda na Unadhimu Daluti - Arusha

Posted on: October 11th, 2021

 

- Afurahishwa na ujio wao wa kujifunza dhana ya maendeleo endelevu ya Viwanda DSM

- Awahakikishia usalama, asema DSM ni sehemu sahihi ndio lango la Kibiashara

- Abainisha namna Mkoa wa DSM unavyojipambanua katika nyanja ya Viwanda

- Brigedia Generali Sylvester Ghuliku ampa KONGOLE  RC Makalla pamoja na zawadi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Octoba 11, 2021 amepokea ujumbe kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Duluti - Arusha, Tanzania ukiongozwa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Brigedia Generali Sylvester Ghuliku

Ujumbe huo umepokelewa na Mhe Makalla pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa Bwana Hashim Rugwa na kupata wasaa wa kufanya mazungumzo katika Ukumbi wa Anatoglo Mnazimmoja - Ilala, Dar es Salaam.

Wakati wa Kujitambulisha Brigedia Generali Sylvester Ghuliku alitambulisha timu ya makamanda alioambatana nao, wakiwemo wazawa na wengine wanafunzi kutoka mataifa rafiki kama Kenya, Uganda, Burudani, Malawi, Egypt, na Rwanda ambapo amebainisha lengo la ujio wao ni ziara mafunzo katika nyanja ya Maendeleo endelevu ya Viwanda Mkoa wa Dar es Salaam.

Mhe Makalla akiongea na ujumbe huo amesema Dar es Salaam ni Mkoa wa Kibiashara una viwanda vingi, ni lango, Bandari kubwa iko hapa, kufanya ziara DSM ni sehemu sahihi.

" Tumeendelea kuvutia wawekezaji kwa kuboresha mazingira ya Kibiashara ikiwemo kuwa na One Stop Center, kuboresha miundombinu, Kuwa na kodi rafiki, Kuondoa urasimu, kuboresha Bandari ya DSM na hilo ni mpongeze sana Rais Mhe Samia Suluhu Hassan " Alisema Mhe Makalla

Mkuu wa Mkoa amesema wakiwa katika Mkoa wa DSM watapata fursa ya Kutembelea EPZA ambapo watajionea viwanda vingi ambayo vinazalisha bidhaa zinazopelekwa nje ya nchi.

Mhe Makalla amebainisha Mkoa huu unajipambanua kwa kuwa na Viwanda vingi vya aina mbalimbali na bidhaa anuai zinazalishwa kwa kuwa maendeleo ni "Process" siku za usoni hata magari yatazalishwa hapa.

Aidha Mkuu wa Mkoa amesema Dar es Salaam ni Salama ujumbe huo kuja Dar es Salaam utajifunza mengi na kwa wale makamanda wa mataifa jirani wakirudi kwao anaamini watakuwa mabalozi wazuri wa maendeleo endelevu ya Viwanda Tanzania hususani Mkoa wa Dar es Salaam.

Brigedia Generali Sylvester Damian Ghuliku amempa KONGOLE Mkuu wa Mkoa Mhe Amos Makalla pamoja na kumkabidhi zawadi mbalimbali kama kumbukumbu kwake.










 





Matangazo

  • RATIBA YA KAZI YA MHE. RC MAKALLA KUANZIA 20 - 26 APRIL,2022 April 20, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Utamilifu (Mock) Mkoa wa Darasa la Saba - 2021 July 30, 2021
  • TAARIFA KWA UMMA BEI ELEKEZI YA MBOLEA March 30, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Dar es Salaam Yaadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani

    May 24, 2022
  • DC Ilala Ataka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kuchukua Hatua kwa Wanaokaidi Maelekezo Wanayoyatoa

    May 19, 2022
  • "Dar es Salaam Mmefanya Vizuri Oparesheni ya Anwani za Makazi na Postikodi" Waziri Nape

    May 18, 2022
  • RC Makalla Apokea Kero zaJumuiya ya Wafanyabiashara Dar es Salaam.

    May 16, 2022
  • Tazama zote

Video

Maelekezo ya RC Makalla juu ya Mapambano dhidi ya majanga ya moto katika masoko DSM.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa