• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makalla Aipongeza China Dasheng Bank

Posted on: October 13th, 2021

 

- Asema Benki hiyo imepata mafanikio makubwa kwa Kipindi kifupi

- Ashuhudia fursa za ajira za vijana wazawa katika Benki hiyo

- Asisitiza Umuhimu wa NGUVU YA HUDUMA katika biashara

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Octoba 13, 2021 ameshiriki hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja katika China Dasheng Bank iliyoko jengo la TTCL Posta - Ilala, Dar es Salaam.

Akiwa katika hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja ya Benki hiyo Mhe Makalla alipata wasaa kusikia taarifa ya Benki hiyo toka ianzishwe.

Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi Mtendaji Bwana Chiwalo amesema Benki hiyo ilianza rasmi *Novemba 2018 hadi sasa Benki ina miaka 2 na mienzi 10

China Dasheng Bank imeanzishwa na wanahisa 6  wawili ni kampuni ya Umma ya watu wa China na wanne ni Kampuni binafsi ya watu wenye asili ya China.

Benki hiyo kwa kipindi cha miaka 2 na mienzi 10 imeweza kupata faida ya Bilioni 5 na imewekeza Bilioni 112 na inauwezo wa kukopesha mteja hadi Bilioni 23.

Baada ya kupokea taarifa hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ameipongeza Benki hiyo kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya muda mfupi.

" Unaposikia faida ya Bilioni 5 ambayo Benki imepata maana yake Serikali imeshapata mapato ambayo ndiyo yanasaidia kutekeleza miradi ya maendeleo, cha kufurahisha Benki hii pia imeajili vijana wa kitanzania na unaendelea kuajili hivyo niwapongeze sana " Alisema Mhe Makalla

Mhe Makalla ameitaka Benki hiyo kuitumia vizuri falsafa ya NGUVU YA HUDUMA ili kuendana na kasi ya ushindani wa biashara za kibenki katika Nchi lakini kwa kufuata kanuni na miongozo ya Benki kuu ya Tanzania (BOT)

Aidha Mkuu wa Mkoa amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe Samia Suluhu Hassan imejipambanua kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji na wafanyabiashara na Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa ndio Mkoa wa Kibiashara amewahakikishia kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na wawekezaji.

Ikiwemo kuondoa urasimu, kuwa na Kodi rafiki, Rushwa, miundombinu mbinu rafiki pamoja Usalama wa Uhakika wakati wote.

Mhe Makalla amebainisha wiki ya Huduma kwa Wateja ni fursa ya kipekee kwa Benki hiyo kukutana na Wateja kusikiliza maoni yao na ushauri juu ya Huduma zinazotolewa na kuweza kuboresha ili kukidhi matakwa ya Wateja hatimaye kupanua wigo wa biashara za kibenki

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa