• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Kunenge Azindua Kampeni ya "Usipime Nguvu ya Maji"

Posted on: May 3rd, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Abubakar Kunenge  amezindua kampeni ya "Usipime Nguvu ya Maji" leo tarehe 03 Mei,2021 kwa kuwataka wananchi wa Mkoa huo kuchukua tahadhari ya Mafuriko ya Maji yaendayo kasi.

Akiongea  na Wahariri wa Vyombo Mbalimbali vya Habari Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema Kufuatia utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) juu ya uwepo wa mvua za Vuli ambazo tayari zimeanza kunyesha na tayari athari za mvua hizo zimeanza kuonekana wananchi wote wanapaswa kuacha kuyajaribu maji yanayotembea ili waweze kuwa salama wao pamoja na Mali zao.

Mhe. Kunenge amesema katika kufuatilia madhara na vifo vinavyotokana na mafuriko, utafiti umeonyesha kuwa zaidi ya Asilimia sabini na tatu ya watu waliopoteza maisha ni kwa sababu ya kujaribu kuvuka maji kwa miguu au kwa kutumia vyombo vya usafiri Kama vile bajaji, pikipiki au magari na hatimaye kusombwa na maji.

Amesema kuwa Maji ya mvua wakati wote yanakuwa na nguvu na kasi ambayo huwezi kuiona kwa macho hivyo amewataka Wananchi kutokudharau maji ambayo hawajui Kina chake,nguvu na kasi yake.

Ameongeza kuwa Mkoa wa Dar es Salaam unazindua kampeni hii ili kutoa tahadhari kwa wananchi wote kuacha kuyajaribu maji yanayotembea kwani yanaweza kuwa na Mambo mengi ndani yake sambamba na ukubwa wa kina chake.

Ili kufikisha kampeni hii kwa wananchi wote Mhe. Kunenge ametoa Rai kwa Vyombo vyote vya Habari, Blogs, Mitandao ya Kijamii, na Wenye Mabango ya Kielektroniki kusaidia kusambaza ujumbe huu kwa watu wote na kwa haraka.

Aidha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imeweka ujumbe huu kwenye Tovuti yake ya www.dsm.go.tz sambamba na kuwapatia "Flash sticks" wahariri waliofika kwenye Mkutano huo.

Mkoa unaendelea kuwaelekeza wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam,hususani wanaoishi katika maeneo ambayo yanakumbwa na mafuriko mara kwa Mara kuendelea kujihadhari kwa kuhamia maeneo salama zaidi.

 Aidha, wananchi wote wanatahadharishwa kutovuka maji ambayo yanatembea kwa kasi kipindi cha mvua kwani yanaweza kusababisha athari mbaya ikiwa ni pamoja na kifo.

Serikali kwa upande wake imekuwa ikijenga Kingo za mito mbalimbali, kujenga madaraja na kujenga Barabara mbalimbali ili kuondoa mafuriko katika Mkoa huu. Alisema Mhe. Kunenge.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa