• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Uso kwa Uso na Bi Martha Aliyelalamika Kupitia Mitandao ya Kijamii Kuidai Hospitali ya Amana

Posted on: March 11th, 2025

 

-Aagiza uhakiki wa madai ya Bi Martha ufanyike haraka kwa kuzingatia nyaraka stahiki.

-Aguswa na utafutaji wa Bi Martha amchangia milioni 2 ya kwake binafsi kama mtaji

-Atoa rai kwa wananchi kuwa na nyaraka stahiki pale wanapofanya kazi na Serikali

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 11,2025 amekutana na Bi Martha ambaye siku za hivi karibuni amesikika kupitia mitandao ya kijamii kuwa anaidai Hospitali ya Rufaa ya Amana zaidi ya shilingi milioni 3 kutokana na kufanya kazi ya kushona nguo za chumba cha upasuaji na kusambaza pazia, kazi ambayo ilifanyika 2017 na 2021.

RC Chalamila amepata wasaa wa kufanya mahojiano na Bi Martha mbele ya waandishi wa habari na watumishi wa Hospitali ya Amana juu ya mchakato mzima wa madai hayo na kumtaka Bi Martha kuleta nyaraka zitakazo muwezesha kulipwa kiasi hicho anachodai huku akimtaka mganga mfawidhi kuharakisha uhakiki wa nyaraka izo ili aweze kupatiwa haki yake anayostahili ambapo amesisitiza kuwa "Malipo ya Serikali hayawezi kufanyika bila kuwa na nyaraka stahiki, hivyo  nyaraka zote zinzotakiwa ziwepo"

Aidha RC Chalamila amemchangia Bi Martha pesa tasilimu milioni 2 za kwake binafsi ili akaongeze mtaji katika biashara zake anazozifanya kwa kuwa ameonyesha kuwa mwanamke mtafutaji licha ya kuwa mjane.

Vilevile RC Chalamila ametoa rai kwa wananchi hasa wale wanaofanya kazi na taasisi mbalimbali za Serikali kuhakikisha wanakuwa na nyaraka stahiki ili kuepuka kuchelewesha malipo yao.

Naye Bi Martha amekiri katika mkataba wake kuna vitu haviko sawa na ameridhika kwa ushauri aliopatiwa na Mkuu wa Mkoa pia amemshukuru kwa kumpatia shilingi milioni 2 kama mtaji wa biashara anayoifanya.

Kwa upande wa Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Amana Dkt Bryson Kiwelu amemshukukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwa karibu na Hospitali hiyo hali  inayochangia kwa kiasi kikubwa utoaji wa huduma bora kwa jamii na amemuakikishia kutekeleza maagizo yake kwa wakati.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa yakagua Miradi ya Maendeleo Wilaya ya Temeke

    May 07, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Maadhimisho ya Mei-Mosi Dar es Salaam.

    May 01, 2025
  • Dkt Hussein Ally Mwinyi Aweka Jiwe la Msingi Barabara ya Kiibada, Mwasonga-Kimbiji

    April 25, 2025
  • RC Chalamila Dar ni Salama Aeleza Mafaniko na Mipango ya Maendeleo ya Mkoa

    April 18, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa