• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Siku ya Mtoto wa Afrika Itukumbushe Wajibu wetu katika Malezi ya Mtoto

Posted on: June 20th, 2024

-Aitaka Jamii kuacha kushabikia vitendo vinavyodharirisha utu wa binadamu 

-Asema mtoto anasitahili kulindwa na kupatiwa haki yake 

-Atoa rai kwa jamii kuacha tabia za kibaguzi kwa watoto wenye ulemavu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Juni 20,2024 ameshiriki maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika akiwa mgeni rasmi katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam Akiwa katika viwanja vya Karimjee 

RC Chalamila alipata wasaa wa kutembelea maonyesho ya kibunifu katika mabanda mbalimbali yaliyoandaliwa katika viwanja hivyo 

Mhe Mkuu wa Mkoa akiongea wakati wa maadhimisho hayo ameitaka jamii kuacha kushabikia vitendo vinavyodharirisha utu wa binadamu kwa mfano tabia ya biashara ya ngono inafanywa na baadhi ya wanawake maarufu kwa jina la “Madada Poa” biashara hiyo imekuwa ikifanyika hadharani bila kujali mila na tamaduni za kiafrika, malezi ya watoto yamekuwa hatarini kutokana na tabia hizo hivyo siyo vema hata kidogo jamii kushabikia vitendo hivyo “ Katika Mkoa wa Dar es Salaam tabia za biashara za ngono hazikubariki “ Alisema RC Chalamila 

Aidha RC Chalamila amesema wakati tunaadhimisha siku ya mtoto Afrika ni vema kutafakari na kujikumbusha wajibu wetu kama jamii katika mambo mbalimbali ikiwemo makuzi na malezi ya mtoto bila kusahau mtoto anastahili kulindwa na kupatiwa haki yake stahiki 

Vilevile RC Chalamila ameitaka jamii kuacha tabia ya kubagua watoto wenye ulemavu ambapo amesema Rais Dkt Samia ni kielelezo kizuri kwa kuwa amekuwa mstari wa mbele kuwekeza katika elimu Jumuishi na hata katika teuzi zake watu wenye ulemavu wamekuwa wakiteuliwa pia kwenye Ajira wamekuwa wakipewa fursa sawa na watu wasio na ulemavu 

Sanjari na hilo RC Chalamila ameelekeza maadhimisho yajayo yafanyike kwa ukubwa zaidi ili kutoa fursa kubwa kwa watoto kufurahia siku hiyo ikiwemo kuwepo kwa michezo ya watoto ya aina mbalimbali Ifahamike kuwa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika hufanyika kila mwaka Juni 16 ambapo huambatana na shughuli mbalimbali za watoto ikiwemo miadahalo kwa lengo la kutathimini changamoto na mafanikio katika mchakato mzima wa makuzi na malezi ya mtoto unaozingatia kulindwa na kupatiwa haki yake

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Ukatili Kinara Migogoro inayohitaji Msaada wa Kisheria-Waziri Mkuu

    June 16, 2025
  • Wananchi Dar Kunufaika na Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia

    June 14, 2025
  • RC Chalamila, Samia Legal Aid Kuzinduliwa Juni 16, 2025 DSM

    June 13, 2025
  • Wataalam Kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Wakutana na Kamati ya Usalama ya Mkoa-DSM

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa