-Amshukuru Rais Dkt Samia kwa kuwa kinara katika kuhakikisha watoto wanapatata misingi bora ya makuzi, malezi na maendeleo yao.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo mapema leo Machi 12,2025 wakati akifungua kikao cha Tathimini ya utekelezaji wa programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto-PJT MMMAM ( Naional Mult-sectoral Early Childhood Development Program) kwa kipindi cha Oktoba- Desemba 2024.
RC Chalamila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa katika kuhakikisha kuwa watoto wanapata msingi bora wa Makuzi, Malezi, na maendeleo yao.
Aidha RC Chalamila amesema kikao hiki cha tathimini ya utekelezaji wa PJT-MMMAM ni fursa adhimu ya kutafakari maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha mienzi mitatu iliyopita, kujadili changamoto na kupanga mikakati ya kuboresha utekelezaji wa Programu kwa kipindi kinachofuata
Kwa upande wa Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila akimkaribisha Mkuu wa Mkoa amesema Programu hiyo ilizinduliwa Dec 13, 2021 ikiwa na lengo la kuhakikisha watoto wanakua na kufikia kiwango cha juu kabisa cha Maelezi, Makuzi na Maendeleo yao ya awali ambapo amesema Mkoa unaendelea kufanya vizuri katika masuala ya lishe bora ambapo hadi sasa Mkoa uko katika kiwango cha chini kabisa cha udumavu hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuondoa kabisa changamoto hiyo.
Vilevile Dkt Toba Nguvila amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa wabunifu, na kutumia mbinu mbalimbali zenye kulenga kuifikia jamii kwa ukubwa wake.
Hata hivyo RC Chalamila amesistiza lazima tuhakikishe kila mtoto anapata hiduma bora za Malezi, Makuzi, na Maendeleo ya Awali ili aweze kufikia kilele cha maendeleo yake Kimwili, Kihisia, Kiroho na kijamii hii inawezekana kwa kuimarisha ushirikiano wetu, kuishirikisha jamii ipasavyo na kuhakikisha rasilimali za kutekeleza programu hii zinapatikana.
Mwisho kikao hicho muhimu kimehudhuriwa na Mganga Mkuu wa Mkoa, mratibu wa programu jumuishi, viongozi wa Dini, waratibu na wataalamu wa programu hii ngazi za Halmashauri, Watalaam kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na wadau wengine wa utekelezaji wa programu ya MMAM kutoka katika mashirika ya kimataifa, Kitaifa na Asasi za Kiraia
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa