• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila: Miradi 36 yenye Thamani ya Tsh 79,255,160,719.44 Kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Dar

Posted on: June 1st, 2025

 

-Mwenge wa Uhuru 2025 katika Mkoa huo utakimbizwa umbali wa KM 357.03

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila wakati akipokea Mwenge wa Uhuru, ukitokea Mkoa wa Lindi leo Juni 1, 2025 katika Stendi ya Mabasi ya mwendo kasi Mbagala Wilaya ya Temeke Jijini humo.

RC Chalamila akiongea wakati wa mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 amesema Mkoa wa Dar es Salaam utakimbiza Mwenge wa Uhuru katika umbali wa KM 357.03 kwa kupitia Miradi 36 yenye thamani ya Tsh.79, 255,160,719.44 (Shilingi Bilioni Sabini naTisa, Milioni Mia Mbili Hamsini na Tano, Laki Moja na Elfu Sitini Mia Saba Kumi na Tisa) Miradi hii ipo iliyokamilika na mingine ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Vilevile, Mwenge wa Uhuru utakapokuwa unapita, utakuwa ukihamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo, upendo, amani, mshikamano na uzalendo kwa Wananchi. Aidha, Mbio za Mwenge wa Uhuru zitahamasisha Wananchi kuhusu kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu kwa maendeleo ya Taifa letu.

RC Chalamila pia amesema Mkoa huo unaungana na Watanzania wote katika kuupokea Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2025 unaolenga kuwaelimisha na kuwahamasisha Wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujitokeza na kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu chini ya kauli mbiu isemayo, JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 KWA AMANI NA UTULIVU. Pamoja na Ujumbe wa kudumu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kuhusu Mapambano dhidi ya: VVU/UKIMWI, Malaria, Dawa za Kulevya, Lishe na Rushwa. Ambapo amesisitiza ni vyema tukaendelea kujikinga na magonjwa hayo hatari pamoja na kupambana na Rushwa na Dawa za kulevya katika jamii zetu.

Sanjari na hilo RC Chalamila amesema Mkoa huo utakimbiza Mwenge wa Uhuru ukianzia Wilaya ya Temeke leo tarehe 01/06/2025 na kufuatiwa na Wilaya ya Kigamboni tarehe 02/06/2025, Wilaya ya Ilala tarehe 03/06/2025, Wilaya ya Kinondoni tarehe 04/06/2025 na kumalizia na Wilaya ya Ubungo tarehe 05/06/2025 kabla ya kuukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkoa wa Tanga tarehe 06/06/2025.

MWISHO Mhe Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam amewakaribisha Wakimbiza Mwenge Kitaifa, ambapo amesema Mwenyezi Mungu awalinde na kuwbariki katika safari yao waliyoianza leo ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru katika Mkoa huo, na ametoa rai kwa Wakazi wa Dar es Salaam kuwa tayari kutoa Ushirikiano mkubwa kuanzia leo hadi siku ya mwisho tutakapo ukabidhi Mwenge huu wa Uhuru kwa Mkoa wa Tanga tarehe 06/06/2025.

 

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Temeke Yang'ara Mwenge wa Uhuru 2025

    June 02, 2025
  • RC Chalamila: Miradi 36 yenye Thamani ya Tsh 79,255,160,719.44 Kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Dar

    June 01, 2025
  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa