• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Kariakoo Kuanza Biashara Saa 24

Posted on: February 24th, 2025

 

-Asema Mataifa yaliyoendelea kote Duniani hufanya biashara usiku na mchana.

-Asistiza DSM kitovu cha biashara lazima biashara ifanyike saa 24,

-Awahakikishia wafanyabiashara usalama wa kutosha.

-Asema baada ya uzinduzi ataunda kamati itakayoongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa kupitia Sheria zinazokinzana na biashara saa 24.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo Februari 24,2025 kwa nyakati tofauti akiwa katika Studio za Crown Media na Kariakoo akiwa anaongea na waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali.

RC Chalamila amesema kwa siku tatu mfululizo kuanzia Februari 25,2025 mpaka kilele chake Februari 27,2025 tunautangazia umma kuanza rasmi kwa biashara saa 24 ambapo Kariakoo ni eneo la uzinduzi lakini wilaya nazo zitaendelea kufanya hivyo Katika maeneo yao ili kuweza kurasimisha biashara saa 24.

Aidha RC Chalamila amesema Mataifa yaliyoendelea hufanya biashara saa 24 ambayo hupanua wigo wa ajira kwa vijana, lakini pia kuongezeka kwa kodi hivyo kwa kuwa Mkoa huu ni kitovu cha Biashara kwa kufanya hivyo vijana watapata fursa za kujiajiri na TRA pia itaweza kukusanya mapato mengi zaidi.

Sambamba na hilo RC Chalamila amewahakikishia wafanyabiashara usalama wa kutosha wasiwe na shaka Dar es Salaam ni salama sana miundombinu ya kiusalama inaendelea kuimarishwa ikiwemo kuwekwa taa na Camera katika Mitaa.

Vilevile RC Chalamila amesema baada ya uzinduzi huo anatarajia kuunda kamati itakayoongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila kwa ajiri ya kupitia sheria zinazokinzana na kufanya biashara saa 24 hasa Sheria ndogo ndogo za Halmashauri za Manispaa.

Mwisho wananchi wamepongeza uamuzi wa Serikali kufanya biashara saa 24 kwa kuwa unafaida kubwa kiuchumi

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa