-Afafanua maboresho makubwa ya miundombinu ya barabara na miradi ya kimkakati
-Awataka wananchi kuendelea kuhamasishana umuhimu wa kulipa kodi
-Awatoa hofu wananchi kuelekea uchaguzi Mkuu 2025 asema Serikali iko imara sana.
-Atoa salamu za heri ya Pasaka, asema DSM ni Salaam sana
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo April 18,2025 amefanya mkutano na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Hotel ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam katika mkutano huo amefafanua mambo mbalimbali ikiwemo usalama wa Mkoa, jumbe zinazozagaa juu ya mafuriko na hatua zinazochukuliwa na Serikali, Kasi ya ulipaji kodi, maboresho ya miundombinu ya barabara pamoja na nafasi ya mkoa kuelekea uchaguzi mkuu 2025.RC Chalamila amesema katika kuboresha miundombinu Serikali mkoani Dar ee salaam imeanza ujenzi wa daraja la jangwani mkandarasi ameanza ujenzi wa karakana ya kuhifadhia hivyo mkandarasi yupo kazini ambapo amewataka wananchi kutokuwa na shaka juu ya ujenzi huo ambao unakwenda kuwa suluhisho la mafuriko eneo hilo
Sanjari na hilo RC Chalamila amezungumzia mpango wa ujenzi wa barabara katika Mkoa huo kupitia mradi wa DMDP ambapo amesema wakandarasi wengi wameshaingia kazini na amewahakikishia wananchi kuwa barabara ambazo bado ujenzi haujaanza ndani ya muda mfupi kazi itaanza pia amesisitiza juu ya mpango wa serikali kuimarisha usafiri wa mwendokasi kupitia wawekezaji binafsi.
Aidha RC Chalamila amezungumzia suala la uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwaka huu na kusisitiza kuwa licha ya tofauti za itikadi za kisiasa zilizopo Mkoa utaendelea kuwa salama kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi na kwamba kila aliejiandikisha Mkoani humo atapiga kura kwa amani na utulivu hivyo amewataka wanasiasa kufanya siasa za kistaarabu kwani Jeshi la polisi litafika kila penye viashiria vya uvunjifu wa amani.Vilevile kupitia mkutano huo ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake kuutaarifu umma kupitia vyombo vya habari Mkuu wa Mkoa huo amezungumzia mpango wa biashara saa 24 na kusisitiza kuwa uwepo wa bandari, uwanja wa ndege wa kimataifa,kituo cha mabasi cha magufuli, umeme na soko lakimataifa la kariakoo ni nyenzo muhimu kufikia lengo la biashara saa 24
Mwisho RC Chalamila amewatakia Kheri ya Pasaka wakristo wote na wakazi wa Dar es Salaam kwa ujumla kusherekea kwa Amani na Utulivu Jeshi la polisi lipo kazini saa 24. Pia amemtangaza Mr Pimbi na wenzake kuanzia leo ni mabarozi wa Mkoa huo wa kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita katika Mkoa huo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa