• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Behewa kwa Behewa Kusikiliza Kero Usafiri wa Treni Kmata- Pugu

Posted on: November 8th, 2023

 

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo leo Novemba 8,2023 amefanya ziara kwa treni za mjini kutoka stesheni ya Kamata kwenda Pugu kuona adha wanazokumbana nazo abiria.

Mhe Albert Chalamila alitumia usafiri huo ili kuweza kuwasikiliza abiria na kuona kero na changamoto wanazokumbana nazo abiria na aliwaeleza kuwa mhe Rais Dkt Samia S. Hassan amewaona jinsi walivyodandia na kuning'inia kwenye treni hivyo amemuagiza  afuatilie kujua ukweli wa Changamoto hiyo.

Aidha Abiria waliokua wakitumia usafiri huo walitumia fursa hiyo kumwelezea RC kero zao zikiwemo matumizi mabaya ya tiketi na ukataji wake, kutokuwepo usimamizi mzuri kwenye mabehewa ya wanafunzi na wazee, kuboreshwa huduma za vyoo, kukosa vituo vya kujikinga na mvua au jua,  na wengine waliomba kuongezewa siku ya jumamosi wapate huduma za treni sababu pilikapilika bado nyingi na pia kuboreshwe geti la kutokea pale Kamata.

Hata hivyo RC Chalamila alisema changamoto hizo kwa sehemu kubwa zitatatuliwa hivyo ameaidi kuendelea kuzitatua na pia kufanya ziara za kushtukiza na za taarifa ili kuwasaidia wananchi.

Pia Mhe Chalamila amemtaka mkandarasi anayejenga barabara ya Pugu ajenge barabara za kando kuepuka wananchi kukwama kwenye foleni na kusababisha watu kuchelewa kazini, "Kipande cha kutoka Banana mpaka mitaa ya Ukonga, magari mengi yanapita kwenye njia moja kwahiyo tumekubaliana mchina aongeze barabara ili magari yaweze kupishana," alisema.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Amina Lumuli aliwaahidi abiria wanaendelea kutatua changamoto wanazopata  na hadi sasa washaongeza 'ruti' na kufikia 8 hivyo abiria watasafiri kwa wakati na salama kufika kwenye shughuli zao au makwao, na alitoa wito kwa wananchi wote wafuate sheria na taratibu usafiri huo.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa