• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Azindua Zoezi la Ugawaji Vyandarua kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi

Posted on: October 18th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Oktoba 18, 2023 amezindua zoezi la ugawaji vyandarua kwa wanafunzi wa shule za msingi Mkoani humo, Uzinduzi ambao umefanyika Katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada Ilala Boma.

Akiongea wakati wa Uzinduzi huo RC Chalamila amesema Serikali chini ya uongozi mahiri wa Rais Dkt Samia imekua ikitekeleza afua mbalimbali za Afya kwa lengo la kulinda Afya za Jamii na ustawi wao, moja ya maeneo yanayotiliwa mkazo ni udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza hususani ugonjwa wa malaria.

Ndio maana Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais- TAMISEMI na wadau wa maendeleo katika kukabiliana na magonjwa hayo imepanga kutekeleza kampeni za ugawaji wa vyandarua kwa wanafunzi wa shule za msingi ndani ya Mkoa zoezi ambalo nimezindua leo

Aidha RC Chalamila amesema kutokana na juhudi mbalimbali na mwitiko kwa wakazi wa Mkoa maambukizi ya malaria yamepungua sana kutoka wastani wa asilimia 6 miaka kumi iliyopita hadi asilimia 0.7 mwaka 2023, Mkoa wa DSM ni moja kati ya mikoa 9 ya Tanzania Bara yenye maambukizi kidogo, pamoja na mafanikio hayo malaria bado ni tatizo kwani mwaka 2022 wakazi 102 waliugua malaria kati yao 14 walithibitika kufariki baada ya kuugua.

Hivyo niwatake viongozi kuendelea kuongeza uelewa kwa jamii na katika taasisi mnazotoka ili wananchi wavipokee na kuvitumia kwa usahihi kila wakati vyandarua hivi ili kujikinga na Mbu waambukizao malaria, vyandarua hivyo vina ukubwa wa futi 5 kwa 6 ambavyo vinatosha kwenye malazi ya walio wengi pia vina viwatilifu vya muda mrefu vinavyoua Mbu, vimethibitishwa kuwa ni salama kwa matumizi ya binadamu, vimetengenezwa hapahapa nchini. "Niwaombe kuendelea kuchukua taadhari dhidi ya malaria kama wataalam wanavyoelimisha ikiwemo kufukia madimbwi pamoja na kuwa tumegawa vyandarua" Alisema Chalamila

Kwa upande wa Mratibu wa Malaria Mkoa Dkt Ford wakati akitoa takwimu za kitaalam za hali halisi ya ugonjwa wa Malaria amesema maeneo ambayo yana kiwango kikubwa cha Malaria ni Luhanga Wilaya ya Ilala na Tudwi Songani kwenye maeneo hayo kati ya watu 100 wanaopimwa malaria zaidi ya 30 huthibitika kuwa na malaria

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Ukatili Kinara Migogoro inayohitaji Msaada wa Kisheria-Waziri Mkuu

    June 16, 2025
  • Wananchi Dar Kunufaika na Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia

    June 14, 2025
  • RC Chalamila, Samia Legal Aid Kuzinduliwa Juni 16, 2025 DSM

    June 13, 2025
  • Wataalam Kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Wakutana na Kamati ya Usalama ya Mkoa-DSM

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa