
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Octoba 09,2025 amezindua programu ya Konekt Umeme, Pika kwa Umeme iliyobuniwa na TANESCO katika viwanja vya Mwembe yanga wilaya ya Temeke.
Programu ya Konekt Umeme, pika kwa umeme ni gharama nafuu, inaufanisi mkubwa, pia umeme unaotumika ni kidogo sana ukilinganisha na nishati zingine.
RC Chalamila amepongeza Wizara ya Nishati, na TANESCO na wadau wote wa maendeleo kwa kuja na wazo hili bunifu lenye lengo la kuongeza upatikanaji wa Nishati safi ya kupikia kwa Watanzania. "Mpango huu ni mwanzo wa zama mpya katika historia ya huduma za umeme nchini unaounga mkono juhudi ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu katika matumizi ya nishati safi".
Kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya umeme kupikia unaifanya jamii ya kitanzania kwenda kwenye viwango bora vya maisha.
Vilevile RC Chalamila amesema ni ukweli usiopingika umeme ni hitaji muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa nchi lakini maendeleo ya mtu mmoja mmoja.

Aidha kwa upande wa Mtendaji mkuu wa TANESCO Bw Lazaro Twange amesema Tanzania kupitia wizara ya Nishati, TANESCO imetangaza rasmi mpango wa kitaifa wa Nishati (Energy Compact) wenye lengo la kuunganisha wateja milioni 8.5 ifikapo 2030 sawa na wateja milioni 1.7 wapya kila mwaka hivyo uzinduzi wa programu ya Konekt Umeme, Pika kwa umeme umefanyika muda muafaka.
Sanjari na hilo amesema mpango huu unatoa fursa kwa mteja kupewa jiko wakati wa kuunganishiwa umeme kisha analipa kidogo kidogo kupitia mfumo wa token hivyo familia nyingi sasa zitaweza kupika kwa ufanisi na kwa gharama nafuu.
Mwisho RC Chalamila amegawa majiko ya Nishati safi ya umeme kwa wananchi mbalimbali na kuwataka kuwa mabalozi kwa jamii ya kitanzania


Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa