• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Azindua Ofisi ya Machinga DSM

Posted on: March 13th, 2025

 

-Amshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kutoa pesa zilizowezesha ujenzi wa ofisi hiyo.
-Awataka machinga na Bodaboda kuitumia ofisi hiyo kuleta matokeo chanya.
-Arudisha tabasamu la Bi Beatrice aliyekumbwa na sakata la kuuzwa nyumba yake
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 13, 2025 amezindua ofisi ya Machinga Mkoa ambayo imejengwa katika eneo la TBA, Kata ya Ndugumbi Magomeni Kota Wilaya ya Kinondoni.
Akifungua ofisi hiyo ya kisasa RC Chalamila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa ya ujenzi wa ofisi ya machinga na mradi mingine inayotekelezwa ndani ya Mkoa huo ambapo amesema furaha ya Rais Samia ni kuona watanzania wanakuwa wanufaika chanya wa miradi hiyo ili kuwa na jamii yenye ustawi.
RC  Chalamila amesema ofisi aliyoizindua itatumiwa na machinga Mkoa pamoja na Bodaboda Mkoa ambapo ameyataka makundi hayo kuitumia ofisi hiyo vizuri ili kuweza kuleta matokeo chanya

Naye Bi Zubeda Masoud akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa Dkt Toba Nguvila amesema ujenzi wa ofisi hiyo ya machinga ni maagizo ya Rais Samia kuwa kila Mkoa uwe na ofisi ya Machinga ambapo alitoa pesa shilingi milioni 10 kupitia OR-TAMISEMI kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo ambayo imezinduliwa leo.

Vilevile kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule amemshukuru Rais Dkt Samia kwa ujenzi wa ofisi hiyo na kuahidi kama Wilaya kumalizia baadhi ya vitu vichache ikiwemo samani na kompyuta ili waweze kufanya kazi zao kisasa zaidi.
Hata hivyo viongozi wa Machinga na Bodaboda kwa nyakati  tofauti wamemshukuru Mhe Rais kwa kulitambua kundi hilo muhimu na wao wako bega kwa bega naye lakini ombi lao ofisi hizo zijengwe pia katika ngazi za Wilaya zote za Mkoa huo

Sambamba na hilo RC Chalamila amerudisha tabasamu kwa Bi Beatrice William ambaye amekumbwa na sakata la kuuzwa nyumba yake ambapo amemhakikishia ofisi yake kwa kushirikiana na TLS imeshaweka pingamizi la kimahakama hivyo nyumba hiyo haitauzwa kwa sasa pia ameongoza changizo kwa ajiri ya kumfariji mama huyo ambapo yeye binafsi ametoa milioni moja huku watu wengine wakijitokeza kwa wingi kumchangia

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa yakagua Miradi ya Maendeleo Wilaya ya Temeke

    May 07, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Maadhimisho ya Mei-Mosi Dar es Salaam.

    May 01, 2025
  • Dkt Hussein Ally Mwinyi Aweka Jiwe la Msingi Barabara ya Kiibada, Mwasonga-Kimbiji

    April 25, 2025
  • RC Chalamila Dar ni Salama Aeleza Mafaniko na Mipango ya Maendeleo ya Mkoa

    April 18, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa