• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC CHALAMILA AZINDUA MFUMO WA USAMBAZAJI GAS YA ORYX KATIKA SOKO LA FERRY

Posted on: August 21st, 2025

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Agosti 21 amezindua mfumo wa kwanza wa usambazaji wa gas ya LPG kwa wingi katika soko la Samaki la kimataifa la Ferry Jijini Dar es Salaam mradi ambao umetekelezwa na KAMPUNI ya ORYX Energies Tanzania  kwa kushirikiana na Serikali.

Mradi huo wa kihistoria ni hatua kubwa katika kuimarisha upatikanaji wa nishati safi kwa wauzaji wa samaki na wajasiriamali wadogo katika soko hilo ambapo sasa mfumo huo unaweza kulipia kadri ya matumizi (PAYG), unaowawezesha wauzaji kulipia gesi wanayotumia tu na hivyo kuondoa gharama kubwa za kujaza mitungi na kupunguza matumizi ya kila siku hadi Sh.45,000.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo huo ambapo limejengwa tanki kubwa ambalo linatumika kusambaza gesi katika majiko ya wafanyabiashara hao, RC Chalamila amesema mfumo huo sasa utawezesha kulipa kulingana na matumizi yako pia mfanyabiashara sasa ana mita yake inayosoma matumizi yake ya kila siku, kabla na baada ya matumizi, hakuna tena kubahatisha, hakuna tena kulazimika kununua mitungi midogo kwa gharama kubwa, vilevile Oryx wamezingatia usalama, kwa kufunga valve ambazo zitatumika kufunga gesi endapo itatokea dharula kwa kila jiko.  Hata hivyo viwango vya matumizi gesi vitafuatiliwa kwa urahisi ili kuhakikisha gesi inaletwa kujaza kwenye hili tanki kubwa kwa wakati huku akieleza gharama imepungua na wafanyabiashara waliokuwa wakitumia hadi Sh.180,000 kujaza gesi kwa siku sasa wanaweza kuokoa hadi Sh.45,000 kila siku. “Kupitia mfumo wa Lipa Kadri Unavyotumia, hili ni suala la kupongezwa sana, hakuna upotevu, hakuna gesi isiyotumika tofauti na zamani ambapo mtungi mdogo mliotumia wakati fulani gesi inabaki kidogo. Usalama wa Juu, hili sina shaka na utalamu wenu Oryx kwenye suala zima la usalama, nafahamu tahadhari zote zimezingatiwa hasa kwa kuweka Vifaa vya kuzima moto nataratibu za dharura zipo tayari"  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Benoit Araman amesema lengo la kuwa na mfumo huo wa kuwa na tanki la gesi katika soko hilo unalenga kupunguza  gharama za kujaza, kupunguza upotevu, na kuongeza ufanisiUsalama  Mfumo usiovuja

Amesema ni mfumo wa kisasa uliofanywa na team ya ufundi ya Oryx gas kwa kuzingatia kanuni za kitaifa na kimataifa, Pia urahisishaji wa Uendeshaji Ugavi endelevu pamoja na ufuatiliaji wa kisasa, na matengenezo madogo.

Awali Katibu Tawala msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Elizabeth Mshote amesma mkakati wa Serikali katika utekelezaji wa ajenda ya Nishati Safi ifikapo 2034 kila wanaposimama watu 10 watu 8 wawe wanatumia Nishati Safi, kwa sasa kila wanaposimama watu 10 watu 3 tu wanatumia Nishati Safi, vilevile takwimu za kitaifa zinasema vifo takribani 33 elfu vinatokea kutokana na madhara ya matumizi ya Nishati chafu, kwa taarifa ya Mkoa katika magonjwa makuu 5 yanayosumbua suala la madhara ya upumuaji ni mojawapo kutokana na Nishati isiyo salama

Katika hatua nyingine aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Ilala Dar es Salaam Mussa Zungu amesema awali wafanyabiashara wa soko hilo walimfikishia mahitaji yao hivyo aliwatafuta Oryx Gas na leo amefurahi kuona umefungwa mfumo huo ambao unakwenda kurahisisha shughuli za wafanyabiashara hao.

Zungu amesema tafiti zinaonesha duniani  kuwa Kuna vifo vingi vinavyotona na Matumizi ya Nishati isio salama hivyo Mradi huu unakwenda kuwa majawabu ya kuimarisha Afya za wadau hao

Matangazo

  • DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 July 17, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA WA DARASA LA SABA MEI, 2025 July 18, 2025
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC CHALAMILA ATANGAZA ZAWADI NONO KWA TAIFA STARS

    August 22, 2025
  • RC CHALAMILA AZINDUA MFUMO WA USAMBAZAJI GAS YA ORYX KATIKA SOKO LA FERRY

    August 21, 2025
  • RAS MHINTE ASISITIZA MAMBO MATATU KUZINGATIWA NA SEKRETARIETI YA MKOA, WAKURUGENZI NA WAKUU WA SEHEMU NA VITENGO WA HALMASHAURI

    August 18, 2025
  • Halmashauri Dar, Zatakiwa Kutumia Jeshi la Akiba.

    August 15, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa