• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Azindua Kongamano la Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia DSM

Posted on: September 30th, 2024

 

-Aishukuru kampuni ya Lake Gas kwa kutoa mitungi 1000 kuunga mkono kampeni ya Mheshimiwa Rais ya Nishati safi.

-Atangaza Tamasha kubwa la Mapishi Septemba 23/2024 kwa kutumia nishati safi.

-Asema tumezindua kampeni ya matumizi ya Nishati safi katika Mkoa, kampeni hii itakua endelevu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila Leo Septemba 12,2024 amezindua kongamano la  matumizi ya Nishati safi ya kupikia katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam ambalo limehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Mameya, Wakurugenzi wa Halmashauri,Watendaji Wakuu wa Taasisi ambata za Nishati safi, Viongozi wa dini na mamia ya mama lishe na baba lishe. Akizindua kongamano hilo RC Chalamila ameishukuru kampuni ya Lake Gas kwa kutoa mitungi 1000 ya Nishati safi ili kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuachana na matumizi ya Nishati chafu badala yake kutumia Nishati safi ya kupikia. "Niwaombe Taasisi, Mashirika na wadau wengine ndani ya Mkoa kuiga mfano wa kampuni ya Lake Gas kuendelea kutoa mitungi zaidi ya gesi ili kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi." Alisema RC Chalamila.

RC Chalamila kupitia kongamano hilo ametangaza Tamasha kubwa la Mapishi kwa kutumia Nishati safi ndani ya Mkoa huo Septemba 23,2024 ambalo litaambatana na Mapishi ya aina mbalimbali kama vile nyama choma,mbuzi choma,samaki choma na pilau vilevile amehamasisha  wananchi kujitokeza kwa wingi na kuahidi kutoa ofa maalum kwa watu 1000 watakaowahi kufika kwenye Tamasha hilo. Eneo la kufanyika kwa Tamasha hilo litatangazwa siku za usoni.

Aidha Mhe.Chalamila amesema leo tumezindua kongamano la matumizi ya Nishati safi ya kupikia katika Mkoa wetu, kampeni hii ni endelevu tukiwa na lengo la kuwafikia wananchi wengi zaidi ili kwenda sambamba na kaulimbiu ya "Jali Afya, Pika Kijanja, Tumia Nishati Safi Okoa Mazingira Kwa Ukuaji wa Uchumi".

Sanjari na hilo RC Chalamila amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa kuratibu upatikanaji wa mitungi ya gesi kutoka Taasisi mbalimbali za serikali kuchangia mitungi kuanzia 200 hadi 300 kabla ya Septemba 30/2024.  

Kwa upande wa muwakilishi wa Mtendaji Mkuu kampuni ya Lake Gas Bw. Stephen Mtemi amesema kampuni ya Lake gas itaendelea kushirikiana na mkoa wa Dar es Salaam kuwafikia wananchi wengi zaidi pia ameishukuru Wizara ya Nishati na wakala wa Nishati vijijini kwa kuwapatia nafasi ya kusambaza majiko ya gesi kwa watanzania wenzetu wa mijini na vijijini hivyo amewaasa watanzania kuendelea kuunga mkono juhudu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa,Dkt.Samia  Suluhu Hassan kwa kutumia Nishati safi.

Mwisho RC Chalamila amewahakikishia watanzania hususani wakazi wa Mkoa huo kuwa hali ya usalama ni shwari, wananchi waendelee na shughuli zao za kila siku za kujipatia kipato pasipo na shaka yoyote.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Ukatili Kinara Migogoro inayohitaji Msaada wa Kisheria-Waziri Mkuu

    June 16, 2025
  • Wananchi Dar Kunufaika na Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia

    June 14, 2025
  • RC Chalamila, Samia Legal Aid Kuzinduliwa Juni 16, 2025 DSM

    June 13, 2025
  • Wataalam Kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Wakutana na Kamati ya Usalama ya Mkoa-DSM

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa