• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Azindua Kitalu Cha Miti Ofisi za Bonde Mto Wami, Ruvu DSM

Posted on: October 27th, 2023

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Oktoba 27 amezindua kitalu cha miti katika Ofisi za Bonde la Mto Wami, Ruvu zilizoko Ubungo Maji Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.

RC Chalamila amepongeza menejimenti ya bonde na wadau wa mazingira katika Mkoa huo kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika masuala yanayohusu mazingira pia wataalam wa Bonde Mto Wami,Ruvu Ofisi ya Dar es Salaam kwa wazo la kuwa na kitalu cha miti chenye miche takribani elfu 55. "Nchi yetu na Dunia kwa ujumla  inapitia Kipindi cha mabadiliko ya tabia ya nchi lazima uwekezaji mkubwa ufanyike kukabiliana na janga hilo hivyo Kinachofanyika hapa ni mwanzo mzuri." Alisema RC Chalamila

Aidha RC Chalamila amesema mazingira yakitunzwa vizuri maji yanapatikana kwa wingi ambayo hutumika majumbani, viwandani, na hata kuzalisha umeme na vingine vinavyofanana na hivyo, ambapo amewataka wote waliokusanyika katika hafla hiyo wakiwemo makandarasi wa usafirishaji mito na vikundi vya machepe kuwa Kielelezo kizuri katika kupanda miti katika mito ili kuzuia ummonyoko wa Kingo za mito vilevile Taasisi kupanda miti rafiki kwa maji na miti ya matunda katika maeneo yao.

Sambamba na hilo RC Chalamila amezitaka Taasisi, Mamlaka na Mashirika pamoja na Halmashauri zote za Mkoa kuja na mawazo ya kibunifu ya kuboresha mazingira hususani "Road Reserve" zilizoko katika Mkoa huo

Kwa upande wa Bi Hadija Faraji Afisa Bonde wa Bonde Mto Wami/Ruvu Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam amesema kitalu kilichozinduliwa leo kina jumla ya miti ya aina mbalimbali ambayo ni rafiki wa maji na matunda takribani elfu 55 na wanategemea kuongeza hadi kufikia laki moja kwa lengo la kuwafikia watu wengi zaidi.

Mwisho Mhe Albert Chalamila amegawa miti kwa wadau mbalimbali wa mazingira waliohudhuria hafla hiyo na kuwataka kupanda miti hiyo na kuendelea kuwa mabalozi wazuri katika utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Ifahamike kuwa moja ya majukumu ya mamlaka ya Bonde la Mto Wami Ruvu ni kufanya ufuatiliaji na tathimini za rasimali maji moja ya utekelezaji wake ni kupanda miti rafiki wa maji kwa lengo la kutunza vyanzo vya maji

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa