-Asema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji wa ndani na nje ili kupanua wigo wa ajira na mapinduzi ya kiuchumi
-Asema katika kila kiwanda ndani ya Mkoa huo kuhakikisha sehemu ya faida inarejeshwa kwa jamii
-Ashiriki kupanda miti kuhamasisha jamii na wadau kutunza mazingira
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Juni 14, 2024 ameungana na mamia ya wafanyakazi katika kiwanda cha Lake Cement LTD Kigamboni katika maadhimisho ya 9 ya wafanyakazi wa kada mbalimbali ikiwa ni utaratibu ambao kiwanda hicho kimejiwekea kwa lengo la kutambua mchango wa wafanyakazi katika uzalishaji ndani ya kiwanda hicho.
RC Chalamila amepongeza uwekezaji uliofanywa na kiwanda cha Lake Cement LTD pamoja na fursa za ajira ambazo zimetolewa kwa vijana wazawa wakitanzania amefurahishwa na jinsi kiwanda hicho kinavyo jali wafanyakazi hadi kufikiria kuwa na siku ya wafanyakazi ambapo amewataka kutokuishia hapo waangalie pia masilahi mengine ya wafanyakazi pamoja na kupandisha mishahara
RC Chalamila amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji katika Mkoa huo ili kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji zaidi wa ndani na nje kwa lengo la kupanua wigo wa ajira na mapinduzi makubwa ya kiuchumi
Aidha RC Chalamila ameelekeza kila kiwanda ndani ya Mkoa huo kuhakikisha kinatoa sehemu ya faida (CSR) kuirejesha kwa jamii ambapo kiasi hicho kitumike katika kutekeleza miradi mikubwa ambayo inamasilahi mapana kwa umma kuliko ilivyo sasa
Sambamba na hilo RC Chalamila ameshiriki zoezi la kupanda miti pamoja na wafanyakazi hao ikiwa ni ishara ya kuelimisha jamii katika utunzaji wa mazingira pia alikabidhi zawadi na tuzo mbalimbali kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho wa kada mbalimbali waliofanya vizuri
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa