Kuelekea sikukuu za Chrismas na Mwaka mpya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amesema ulinzi na usalama umeimarishwa ili kuhakikisha wananchi hususani wakazi wa Mkoa huo wanakuwa salama katika kipindi chote cha sikukuu na baada ya sikukuu, pia amewataka wazazi na walezi kusimamia vema usalama wa watoto kwa kutowapeleka kwenye maeneo hatarishi.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Disemba 23,2024 katika Hotel ya Johari Rotana jijini Dar es salaam wakati akitoa salamu za sikukuu za Chrismas na Mwaka mpya amesema Mkoa kupitia jeshi la polisi umeimarisha ulinzi ambapo ameitaka jamii kushirikiana na serikali kudumisha amani ya Mkoa huo na Taifa kwa ujumla
Aidha Kupitia salamu hizo za sikukuu RC Chalamila amewatoa shaka wananchi wa Mkoa huo kuhusiana na miradi ya ujenzi wa barabara kupitia DMDP ambayo imeonekana kuchelewa ambapo amesema miradi hiyo imeshakabidhiwa kwa wakandarasi na inatarajia kuanza mapema januari mwaka 2025 huku pia akieleza mipango ya kumaliza changamoto ya upatikanaji wa maji safi.
Vilele RC Chalamila amezungumzia mkakati wa kuanza kwa shughuli za kibiashara saa 24 eneo la Kariakoo ambapo amesema zoezi hilo litazinduliwa rasmi mwezi januari 2025 ambapo wakuu wa wilaya,wakurugenzi na maafisa biashara wanapaswa kuainisha maeneo ambayo biashara zinaweza kufanywa saa 24 ikiwwmo eneo la kariakoo
Sanjari na hayo Chalamila amezungumzia mikakati ya Mkoa huo kupokea wanafunzi wa chekechea, darasa la kwanza na kidato cha kwanza na kueleza kuwa serikali imeendelea kuwekeza fedha ili kufikia malengo ya elimu hivyo ambapo amehimiza wafanyabiashara kulipa kodi ili malengo hayo yaweze kutimia
Mwisho akijibu maswali ya waandishi wa habari RC Chalamila ameeleza mipango ya kuboresha huduma za usafiri wa mwendokasi maarufu BRT ambao kwa sasa amesema idadi ya mabasi haitoshelezi , pia amehimiza madereva kutoingilia njia za mabasi ili kuepuka ajali na amesisitiza wananchi kutovamia maeneo kiholela kufanya biashara
Ifahamike kuwa utaratibu huu wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kutoa salamu za sikukuu za mwisho wa mwaka imekuwa na nafasi kwa mkuu wa mkoa kuelezea maendeleo ya mkoa huo na changamoto zilizopo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa