-Mosi Aagiza Eneo la Feri kuwa Safi
-Pili Mchakato wa kumpata Mwekezaji Mkubwa wa dampo uharakishwe
-Tatu Barabara ya Feri kwenda Hyatt, Johari Rotana mpaka stesheni itafungwa kwa baadhi ya vyombo vya usafiri
-Nne Katibu Tawala wa Mkoa kusimamia watendaji wote kuanzia TPA, Temesa kuja Jiji maeneo hayo yawe safi
-Tano Barabara zitakazotumiwa na Marais kwa ajili ya mazoezi ziwashwe taa
-Sita Kibaka yoyote atakayekamatwa apelekwe maabara
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila Leo tarehe 11 Januari 2025 ameshiriki katika zoezi Maalumu la usafi wa Mji pamoja na Vyombo vya Usalama, Viongozi wa Mkoa, Wilaya, Halmashauri na Taasisi za Umma lililofanyika katika Wilaya ya Ilala.
Akiwa katika zoezi Maalumu la Usafi RC Chalamila ametoa Maelekezo *Sita* ya kuzingatia kuelekea Maandalizi ya ujio wa Marais wa Afrika ikiwa ni pamoja na:-
Mosi, Eneo la feri linapaswa kuwa safi ambapo Mhe. Chalamila amesema Soko Hilo kwa muda mrefu limekuwa haliridhishi katika usafi hivyo kama atagundua bado hali ni mbaya tarehe 23- 25 atapafunga na kuwaleta Jeshi, Polisi, Jkt, Zimamoto, Uhamiaji watafanya usafi mpaka pale watakapojifunza wafanyabiashara hao namna ya kufanya biashara na kutunza mazingira
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ameagiza Mchakato wa kumpata Mwekezaji Mkubwa wa Dampo uharakishwe mara Moja ili dampo lipate mwekezaji Mkubwa anayejitambua anayeweza kuzalisha ajira, gesi, na mbolea
Vile vile RC Chalamila ameongeza kuwa Barabara ya feri kwenda hyati, Johari Rotana mpaka stesheni itafungwa *kwa baadhi ya vyombo vya usafiri* na kuelekezwa vipite wapi ili wageni wetu watakapokuwa hapa kusiwe na foleni kubwa
Aidhaa, Mhe. Mkuu wa Mkoa amemuagiza Katibu Tawala kuwasimamia watendaji wote wa maeneo ya kuanzia TPA kuja Temesa kuelekea Jiji kuwa yawe safi
Wakati huo huo RC Chalamila amesisitiza kuwa Barabara zitakazotumiwa na Marais kwa ajili ya mazoezi ziwashwe taa ili vibaba wadogo wadogo waweze kuwa na aibu kutokana na taa zinazowaka
Mwisho Mhe.Chalamila akasisitiza kuwa kibaka wote kuanzia Leo atakayekamatwa apelekwe maabara ili kiwe chombo Cha kufundishia kwa wanafunzi wanaotaka kuja kuwa wezi (watakaojifunza kuwa wizi haustahili katika Jiji la Dar es Salaam)
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa