• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Atoa Maelekezo Mahususi Ukanda wa Kibiashara Kariakoo

Posted on: July 10th, 2024

 

 

-Ataka kutekelezwa haraka kwa maelekezo yake ili kufikia adhima ya serikali kufanya biashara saa 24

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 10,2024 amefanya kikao na viongozi wa wafanyabiashara pamoja na viongozi wa Serikali, Taasisi, Mashirika na wataalam kutoka ofisi yake, katika ukumbi wa Arnatoglo Mnazi mmoja Wilaya ya Ilala Jijini humo.

RC Chalamila amesema Soko la Kariakoo ni Soko la Kimataifa na Serikali imefanya na inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa,ambapo ujenzi na ukarabati wa Soko la Kariakoo kwa gharama ya zaidi ya Bilioni 28 ni moja ya ushaidi tosha wa uwekezaji huo.

Aidha RC chalamila ameagiza kufanyika kwa yafuatayo: mosi kuanza kupendezesha Soko la Kariakoo,kuweka mazingira yanayovutia ikiwemo kuwapanga vizuri wafanyabiashara hususani wadogowadogo,pia usafi wa mazingira unaoendana na kuweka vizuri mifumo ya maji taka na usafi kwa ujamla wake ambapo amesema wakandarasi wenye uwezo na vifaa vya kisasa ndiyo wanatakiwa.

Vilevile DART ambaye ni msimamizi wa huduma za mabasi ya haraka kuweka mkakati kabambe wa kuhakikisha mabasi hayalali yanafanya kazi saa 24, pia katika ukanda wa Kariakoo kuanzisha Kituo cha pamoja cha kutoa huduma kwa wafanyabiashara, lakini kwa upande wa LATRA RC Chalamila ameitaka kuangalia Route za mabasi yanayo kuingia na kutoka ukanda wa kariakoo.

Sanjari na hilo RC Chalamila amezitaka taasisi na mashirika katika mkoa huo kuchangia taa za barabarani ili kuwezesha usalama nyakati zote, pia kufungwa CCTV Camera aidha amewataka vyombo vya dola kijipanga vizuri kuimarisha ulinzi na usalama saa 24.

Sambamba hilo Mhe Mkuu wa Mkoa ameagiza uhamiaji kufanyia kazi wageni wanaojishughulisha na kazi ambazo zingeweza kufanywa na wazawa vilevile taasisi za fedha kuanza kujipanga kuwa na dirisha la kutoa huduma hiyo saa 24 vilevile TANROAD, TARURA kuhakikisha barabara za ukanda wa soko la kariakoo zinakuwa nzuri bila mashimo “ Rais Samia matarajio yake ni kuona watu wengi wanakuwa busy na mifumo ya biashara” Alisama Chalamila.

Mwisho Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt Toba Nguvila amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kusimamia kwa weledi mkubwa maelekezo yake kwa masilahi mapana ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa