• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Ataka Wakazi wa Jimbo la Ubungo Kuunga Mkono Juhudi za Serikali

Posted on: August 14th, 2024

 

-Asema Rais Samia ametoa pesa nyingi za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

-Atembelea na kukagua Soko la ndizi mabibo, ujenzi wa barabara KM 0.3 Makoka pamoja na kufanya mkutano wa hadhara Viwanja vya Shule ya Msingi mabibo Makuburi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila leo Agosti 14,2024 amefanya ziara katika jimbo la Ubungo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na Kuzungumza na wananchi wa wilaya hiyo ambapo amepata nafasi ya kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi papo hapo

RC Chalamila akiongea na wananchi kwa nyakati tofauti amewataka kuunga mkono juhudi za Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa maendeleo anayoyafanya yanaonekana katika maeneo mbalimbali ya Nchi hususani Wilaya ya Ubungo."Mhe Rais ametoa pesa nyingi katika Jimbo la ubungo ndiyo maana miradi mingi inatekelezwa" Alisema Chalamila.

Aidha RC Chalamila amekagua Soko la ndizi ambalo kwa muda mrefu lilikuwa halina faida kwa serikali lakini baada ya kurejeshwa mikononi mwa Halmashauri ya Ubungo sasa pesa zinaonekana na tayari maboresho ya soko hilo yameanza kufanyika.

Vilevile Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Bw. Jaffary Juma Nyaigesha amesema Halmashauri inasimamia Soko hilo kwa weledi mkubwa ambapo amewaahidi wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la ndizi mabibo kuwa fedha zao zipo mikono salama na zitasaidia katika mikakati ya mpangilio sahihi wa sokoni tena wenye tija watu wengi.

Sanjari na hilo RC Chalamila alitembelea barabara ya Makoka ambapo aliwataka wakandarasi kukamilisha mradi huo kwa ubora,viwango na kwa wakati ili kuepusha athari zinazoweza kuletwa na mvua hapo baadaye.

Mwisho Wananchi wa Jimbo la Ubungo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe Hassan Bomboko walimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa ziara yake na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kuboresha maisha yao ambapo wamesema ziara hiyo imeacha matumaini mapya na ari ya maendeleo miongoni mwa wakazi wa Wilaya ya Ubungo

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa