• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

Posted on: May 28th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametoa muda wa wiki mbili kwa uongozi wa wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga eneo la kariakoo kuanza kufungua njia ili kuruhushu shughuli za kibiashara kufanyika kwa ufanisi wakati serikali ikielekea kufanya uzinduzi wa soko jipya la Kariakoo

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari  RC Chalamila amesema wanapoelekea kwenye uzinduzi wa soko jipya ni muhimu kwa Machinga kariakoo kufungua njia za kuingia ili kupeleka bidhaa kwenye soko jipya la kariakoo kwani soko hilo limeshakamilika kwa asilimia 98 hivyo ni muhimu njia zikawa wazi na ametoa muda wa wiki mbili kuanzia leo Mei 28,2025.

RC Chalamila amesema kuwa wafanyabiashara wadogo watakaoondoshwa kwenye njia hizo zinazopaswa kufunguliwa watapelekwa kwenye maeneo maalum yanayotengwa kwani Serikali inatambua uwepo wa machinga kwenye eneo hilo kama ambavyo wizara ya TAMISEMI imeshaelekeza

Aidha RC Chalamila amezungumzia suala la wafanyabiashara waliokuwepo kwenye Soko la Kariakoo hapo awali kabla halijaungua ambapo amesema wote waliokuwepo kuhakikiwa na watajejeshwa kama ambavyo Rais Dkt Samia alivyoelekeza na watapaswa kufuata taratibu ikiwemo kujaza mikataba na kujiandaa kulipa kodi na kwamba Mkoa huo umefanikiwa kuondoa udalali wa upangishaji maeneo na sasa mfumo wa kidijitali ndio unatumika.

Kwa upande wake Meneja Mkuu shirika la Masoko Kariakoo Ashrafu Abdulkarim amesema Shirika hilo linaendelea kuratibu wafanyabiashara waliokuwepo kurejea kwenye Soko hilo ambapo kwa idadi walikuwa 1520 lakini hadi sasa waliojisajili kwenye mfumo na kujaza fomu ni wafanyabiashara 1159 na kusema kuwa maeneo mengine ya wazi yaliyobaki yatatangazwa kupitia mfumo wa TAUSI ili yapate wapangaji

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa