• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Ataka Kasi ya Ukusanyaji Mapato DSM

Posted on: October 31st, 2023

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Oktoba 31,2023 ameongoza kikao maalum cha tathimini ya ukusanyaji mapato katika Mkoa huo kwa kipindi cha robo mwaka wa fedha 2023/2024 ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Arnatoglo Mnazimmoja na kuhudhuriwa na wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, TRA na Sekretarieti ya Mkoa ikiongozwa na Katibu Tawala Mkoa Bi Rehema Madenge.

RC Chalamila katika kikao hicho alipata wasaa wa kusikiliza wasilisho la hali halisi ya mapato katika Halmashauri na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA na kuwataka kuongeza Kasi ya ukusanyaji mapato, kuthibiti matumizi, kuwa na ubunifu wa kubuni vyanzo vipya vya mapato pia kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato na kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kulipa kodi. " Kila Halmashauri ijipange kukusanya zaidi ya makisio yao waliyojiwekea kwa mwaka, mfano Jiji makisio yake yalikuwa ni Bilioni 89 lakini uko uwezekano mkubwa wa kukusanya zaidi ya Bilioni 120 kutokana na mikakati yake" Alisema RC Chalamila.

Aidha RC Chalamila amesema vikao vya tathimini ya mapato kuanzia sasa vitakua vinafanyika mara kwa mara na ratiba maalum ya vikao hivyo itatolewa na katibu Tawala wa Mkoa.

Vilevile Mhe Mkuu wa Mkoa amesema makusanyo ya mapato yaendane na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo ni aibu kwa Mkoa huu ambao kila kitu kipo unashindwa kukamilisha miradi ya maendeleo.

Kwa upande wa Katibu Tawala wa Mkoa Bi Rehema Madenge amepongeza Halmashauri kwa asilimia kubwa zimefikia lengo la robo ambapo amewataka kuendelea kusimamia vema mapato na matumizi, kuziba mianya ya upotevu wa mapato katika mifumo, kutenga asilimia 10 vilevile Mkoa huo unatakiwa kuwa na miradi ya mfano, mizuri na yenye tija kwa masilahi mapana kwa Umma

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa