• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Ataka Jamii Kutafsiri kwa Vitendo Maendeleo Yanayofanywa na Rais Dkt Samia

Posted on: February 10th, 2025

 

-Asema kwa mfano Rais Dkt Samia ameboresha kwa kiasi kikubwa sekta ya elimu Je? jamii na wadau wengine wa elimu wanafanya nini ili kuinua viwango vya ufaulu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amewataka viongozi na wataalamu Mkoani humo kutafsiri vema na kwa vitendo maendeleo yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya elimu na afya ili iwe na tija kwa jamii hususani katika kuinua ufaulu wa wanafunzi kwenye shule ambazo hazifanyi vizuri

RC Chalamila akizungumza leo Feb 10, 2025 Wilayani Temeke Jijini Dar es salaam katika mkutano na wadau mbalimbali wa elimu amesema Serikali chini ya Rais Dkt Samia imekuwa ikiimarisha miundombinu ya elimu na mazingira ya kufundishia na kujifunzia hivyo ni muhimu kwa kila mdau wa elimu ikiwemo wazazi, viongozi pamoja wataalamu kujielekeza kwenye kusaidia watoto ili kuinua viwango vya ufaulu kwa wanafunzi

Aidha RC Chalamila amesema kuwa badala ya kutazama sababu chache zinazotolewa na kuonekana kusababisha ufaulu kuwa hafifu ni muhimu kufanya utafiti wa kina na kuhakikisha wazazi wanashirikishwa ipasavyo kwenye kuinua ufaulu wa wanafunzi ili  ndoto za Rais Dkt Samia zitimie na fedha nyingi anazozitoa kuimarisha miundombinu ya elimu zitimize lengo husika.

Vilevile RC Chalamila amesema hivi karibuni Serikali Mkoani humo inatarajia kufanya mkutano utakaojumuisha wazazi na wadau wengine wa elimu ili kujadili kwa pamoja na kuimarisha ushirikishwaji wa wazazi kwenye masuala ya elimu.

Naye Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe Sixtus Mapunda amesema wanakwenda kujielekeza kwenye kutafuta chanzo cha changamoto ya wanafunzi kutofanya vizuri kwenye mitihani yao ili kupata suluhisho la kudumu kwenye elimu na kwamba pamoja na kuendelea kuimarisha miundombinu watashirikisha wazazi  na wahitimu wa vyuo vikuu kwenye kada ya elimu

Sanjali na hilo mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Abdallah Mtinika ametaja changamoto ya lugha ya kingereza kama kikwazo cha ufaulu kwa wanafunzi huku Afisa elimu Mkoa wa Dar es salaam Bwana Gift Kyando akizungumzia changamoto ya usafiri kwa wanafunzi wanaosoma shule za mbali ambao wamekua wakiachwa vituoni na magari.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa