• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Apokea Melivita ya Matibabu ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Maarufu kwa Jina la Peace Ark

Posted on: July 16th, 2024

 

-Atoa rai kwa wakazi wa Dar es salaam na watanzania kujitokeza kwa wingi kupatiwa matibabu


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 16,2024 amepokea Melivita ya matibabu iitwayo Peace Ark ya Jeshi la ukombozi la watu wa China katika Bandari ya Dar es Salaam.  

RC Chalamila akiongea wakati wa mapokezi hayo amesema Melivita hiyo itakuwepo katika Mkoa wetu kutoa huduma za kitabibu kwa wakazi wa mkoa huu na watanzania kwa ujumla kuanzia tarehe l16 Julai, 2024 hadi tarehe 23 Julai,2024 ambapo leo Julai 16, 2024 ni siku maalum ya uzinduzi, na kuanzia tarehe 18-23 Julai 2024 ndyio siku rasmi ya kuanza kutoa matibabu kwa wananchi. Huduma hizo za kitabibu zinatolewa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka sitini(60) ya ushirikiano kati ya Tanzania na China na maadhimisho ya miaka sitini (60) tangu kuanzishwa kwa JWTZ tarehe 01 Septemba,1964.

Aidha RC Chalamila amesema huduma za kitabibu zinazotarajiwa kutolewa ni pamoja na vipimo, tiba za kawaida pamoja na upasuaji wa kawaida, magonjwa ya kina mama, mifupa, njia ya mkojo, macho, pua, koo, meno, moyo, utumbo pamoja na ngozi zilizoungua na moto ambapo matibabu hayo yatatolewa kwa ushirikiano wa wataalamu wa Afya wa JWTZ, Hospitali ya Taifa Muhimbili,Tumbi,Amana,Mwananyala,Temeke,na Jeshi la China.

Vilevile kutakuwa na kikundi cha Madaktari Bingwa watakaokuwa wanakwenda kutoa matibabu kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mbagala , Hospitali ya Lugalo na Kunduchi  ,Hospitali ya Amana, Bunju, Mwananyamala  na Temeke pamoja na maeneo mengine ambayo ratiba rasmi itatolewa na JWTZ.   

Sanjari na hilo amesema wananchi watakaokwenda Bandarini kwenye Meli hiyo kwa ajili ya kupata matibabu wanataarifiwa wapitie geti namba mbili(2) la Bandari ya Dar es salaam.

Mwisho  RC Chalamila amesema Matibabu hayo yatatolewa bure, hivyo ametoa rai kwa wananchi wanaohitaji huduma hizo kujitokeza kwa wingi kuitumia fursa hiyo  ya kitabibu.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Temeke Yang'ara Mwenge wa Uhuru 2025

    June 02, 2025
  • RC Chalamila: Miradi 36 yenye Thamani ya Tsh 79,255,160,719.44 Kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Dar

    June 01, 2025
  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa