• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Aongoza Maadhimisho ya Mei-Mosi Dar es Salaam.

Posted on: May 1st, 2025

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameongoza maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani Mei Mosi Mkoani humo na kuwataka wafanyakazi kufanya kazi kwa umahiri na uadilifu huku wakiamini kuwa Serikali inawapenda na inaendelea kushughulikia changamoto zaoRC Chalamila akizungumza Jijini Dar es salaam leo  katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei Mosi yaliyofanyika kimkoa kwenye viwanja vya Tanganyika Perkas, amewataka wafanyakazi kufanyakazi kwa uadilifu bila kufanya ubadhilifu kwenye utendaji wao ili kila mwananchi anufaike na utumishi wao kwani Serilali inaendelea kushughulikia changamoto zao
Aidha RC Chalamila ameeleza kusikitishwa na baadhi ya watumishi  wasiokuwa waadilifu wanaopelekea baadhi ya wananchi kuichukia Serikali  kutokana kutowatendea haki pale wanapohitaji huduma mbalimbali ambapo amesema kutowavumilia watumishi wa aina hiyo endapo tabia hizo zitajitokeza hatua za kisheria zitachukuliwa,ametolea mfano watumishi waliovamia saluni ya mmoja wa wakazi wa Mkoa huo na kumuambia anakosa la kutoa huduma bila kukamilisha taratibu za kupima afya kwa wahudumu hivyo waliwataka kulipa shilingi laki sita ambapo amesema huo sio utumishi bora wa umma.
Vilevile RC Chalamila ametumia maadhimisho hayo kuwataka wafanyakazi Mkoani humo kushiriki uchaguzi mkuu ili kupata viongozi bora watakaosaidia kuboresha maslahi ya wafanyakazi na kuleta maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule akizungumza kwa niaba ya wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Dar es salaam amesema katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt Samia ameendelea kuifungua nchi kiuchumi hivyo amewataka wafanyakazi kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais kwa kuendelea kufanya kazi vyema huku akiwataka pia kushiriki uchaguziAkisoma risala kwa niaba ya wafanyakazi Mkoa wa Dar es salaam Katibu wa Chama cha mawasiliano na Uchukuzi Tanzania COTWUT Meshack Sarota amesema wanaamini Serikali sikivu ya awamu ya sita itaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kuongeza mishahara ikiwemo kwenye sekta binafsi,kupunguza kodi,kupunguza gharama za vifurushi kwenye bima ya afya na kuhakikisha wafanyakazi wote wanapata huduma bora za afya kupitia bima.
Sanjari na hayo ameomba Serikali kuimarisha usalama na Afya mahali pa kazi na kuondosha mikataba ya kazi ambayo ni kandamizi kwa wafanyakazi
Kupitia maadhimisho hayo wafanyakazi waliofanya vizuri kwenye utumishi wao wa mwaka mzima wamepatiwa zawadi ya fedha taslimu ambapo baada ya kupatiwa zawadi wafanyakazi hao wameeleza furaha yao kwa Serikali
Mwisho maadhimisho hayo yamebeba kaulimbiu isemayo "Uchaguzi mkuu 2025 utuletee viongozi wanaojali haki na maslahi ya wafanyakazi sote tushiriki"

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa