• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Aongoza Kikao Cha Tathmini ya Lishe -DSM

Posted on: August 21st, 2024

 

-Asema lishe bora ni muhimu kwa ustawi wa jamii hapa Nchini.

-Awataka wadau kushirikishana na serikali kuwekeza katika afua za lishe ili kupunguza idadi ya watoto wenye upungufu wa damu.

-Asisitizia jamii kuchukua tahadhari kwa kujikinga na maradhi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila Leo Agosti 20,2024 ameongoza kikao Cha tathmini ya lishe katika ngazi ya mkoa katika Ukumbi wa Anartoglo- Ilala, kwa lengo la kujadili changamoto na mafanikio yaliyopatikana katika jitihada za kuboresha hali ya lishe mkoani humo hususani kwa watoto na wanawake wajawazito.

RC Chalamila amepongeza serikali chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kulipa kipaumbele suala la lishe na kusaini mkataba wa utekelezaji wa afua za lishe na Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa yote 26 ili kuwapima utendaji kazi wao katika kusimamia utekelezaji wa makubaliano yaliyowekwa na kuagiza idara zote na sekta zote kulichukulia suala Hilo kwa uzito wake.

Aidha RC Chalamila alisisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za haraka na za makusudi katika kuboresha lishe, akieleza kuwa tatizo la udumavu bado ni changamoto kubwa inayokabili jamii. Aliwahimiza viongozi wa wilaya na wakuu wa idara kushirikiana kwa karibu zaidi na wadau wengine kuhakikisha mipango iliyopo inatekelezwa kwa ufanisi.

Vilevile Mhe. Chalamila ameendelea kuikumbusha jamii kuchukua tahadhari kwa lengo la kujikinga na maradhi kama vile kufanya usafi binafsi na usafi wa Mazingira pamoja na afua za Kinga dhidi ya UKIMWI,Kifua kiku,Malaria na Magonjwa yasiyoambukiza pamoja na ufanyaji wa mazoezi ya viungo vya mwili.

Sanjari na hilo Katibu Tawala wa Mkoa Dkt. Toba Nguvila ametoa rai kwa wadau wa maendeleo kuwa waangalizi juu ya vyakula na mwenendo wa Clinic kwa kinamama wajawazito  na kupinga matumizi ya pombe pamoja na madawa ya kulevya ili kuepusha athari kwa mtoto

Mwisho,kikao kilihitimishwa kwa makubaliano ya kuimarisha mikakati ya lishe kwa kushirikiana na wadau wote muhimu, huku wakilenga kuboresha zaidi utoaji wa huduma za lishe katika vituo vya afya na katika ngazi za halmashauri

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa