• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Amtaka Mkandarasi Barabar ya Kitunda, Kivule, Msongola Kuanza Ujenzi Mara moja

Posted on: March 25th, 2025

 

-Asema  ajaridhishwa na mwenendo wa kazi, kwa kuwa mpaka sasa haoni vifaa vyovyote eneo la mradi.

-Asisitiza wananchi wa Kitunda, Kivule, Msongola na majohe njia 4 wanataka kuona  barabara za lami sio vinginevyo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 24, 2025 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kitunda, Kivule Msongola na Majohe njia 4 ambayo toka makataba wa ujenzi usainiwe mwaka jana mpaka sasa Mkandarasi amejenga Camp tu na vifaa vya ujenzi havionekani licha ya kuwa alishalipwa sehemu ya fedha za kuanza ujenzi huo.

RC Chalamila amemtaka Mkandarasi kuanza ujenzi huo mara moja, atakapokuja tena aone mabadiliko makubwa la sivyo hatakuwa na uvumilivu tena vilevile amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kumuandalia Mkutano wa hadhara ili aweze kuongea na wananchi  wamueleze kero zao. "Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imejipanga vizuri katika kuboresha huduma mbalimbali za jamii ikiwemo barabara ili kuwa na jamii yenye ustawi hivyo wakazi wa eneo hilo wakae mkao wa kula" Alisema Chalamila.

Vilevile RC Chalamila amesisitiza Mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni wa kipekee kila kitu kihitaji pesa na ili upate pesa lazima uhangaike muda wote na kuhangaika kunahitaji amani hivyo kila mmoja ana kila sababu ya kuilinda amani kwa nguvu zote.

Naye Meneja TARURA Mkoa Mhandisi Jofrey Mkinga amesema kwa mujibu wa mkataba Mkandarasi huyo mpaka sasa yuko nje ya muda kwa miezi miwili kitu ambacho amekifanya eneo la mradi hadi sasa ni kujenga Camp tu hivyo utekelezaji wa mradi uko chini.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa hufanya ziara katika Wilaya hiyo ambapo amesema changamoto za wakazi wa eneo hilo ilikuwa ni barabara pamoja Vituo vya Afya hivyo anamuomba Mkuu wa Mkoa kumpelekea salaam za wana Ilala Mhe Rais kwa kutoa pesa za ujenzi wa barabara na kituo cha afya ambacho ujenzi wake unaendelea.

Mwisho mwenyekiti wa Mtaa wa Mbondole Bwana Thomas Nyanduli amesema anajisikia furaha kuona mkuu wa Mkoa amekuja kukagua mradi huo hivyo ameshukuru na kupongeza kwa dhati kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na walioko chini yake hususani Mkuu wa Mkoa.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa yakagua Miradi ya Maendeleo Wilaya ya Temeke

    May 07, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Maadhimisho ya Mei-Mosi Dar es Salaam.

    May 01, 2025
  • Dkt Hussein Ally Mwinyi Aweka Jiwe la Msingi Barabara ya Kiibada, Mwasonga-Kimbiji

    April 25, 2025
  • RC Chalamila Dar ni Salama Aeleza Mafaniko na Mipango ya Maendeleo ya Mkoa

    April 18, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa