• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Akutana na Wadau wa Nishati ya Mafuta Dar

Posted on: November 7th, 2025

 

-Aongoza mjadala mpana kuhusu ulinzi na namna bora ya uuzaji wa Nishati ya mafuta.

-Atoa pole kwa wakazi wa mkoa huo hususani wadau wa Nishati ya mafuta

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Novemba 07,2025 amekutana na wadau wa Nishati ya Mafuta ya Disel na Petroli katika kikao maalum ambacho kiliratibiwa na EWURA katika ukumbi wa Jengo la PSSSF Sinza Wilayani Ubungo

RC Chalamila katika kikao hicho ameongoza mjadala mpana wa ulinzi na usalama wa vituo vya kuuzia Nishati mafuta kufuatia tukio la hivi karibuni la uhalifu lililofanywa na vikundi vya vijana wasio itakia mema nchi yetu ambapo vituo mbalimbali vya mafuta vilichomwa moto uliopekea hasara kubwa kwa wafanyabiashara hao ambapo kupitia mjadala huo wadau wamepata fursa ya kutoa maoni na ushauri wenye lengo la kuimarisha sekta hiyo kufuatia athari zilizotokea.

Aidha RC Chalamila amewapa pole wadau hao na kuendelea kuwatia moyo kuwa Serikali bado iko bega kwa bega na wafanyabiashara hao kwa kuwa wana mchango mkubwa katika mnyororo wa uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini pia Taifa kwa ujumla.

"Ni vema sasa kuratibu vizuri uuzwaji wa mafuta kwenye vidumu, kwa kuwa huwezi kuzuia kabisa kwa kuwa yako maeneo au vyombo vinavyotumia nishati hiyo huitaji mafuta yapelekwe kama vile minara ya simu na boti" Alisema Chalamila

Vilevile RC Chalamila amewataka wadau na jamii kwa ujumla kuendelea kutoa elimu kwa vijana hususani katika makundi yao kama vile pikipiki,  na bajaji kutambua umuhimu wa kulinda na kudumisha amani katika Mkoa huo kwa kuwa Dar es Salaam inahudumia nchi nyingi zisizo na bandari pamoja na kuwepo kwa shughuli nyingi za kujipatia kipato na huduma za afya za kibingwa pia amesistiza "kwamba kama kuna Jambo lolote, makundi ya Vijana. Wazee na akina mama tukutane tujadili, wapi tunadhani turekebishee ili asiwepo mwenye kinyongo, na kuendelea kuiweka nchi yetu ikiwa moja".

Mwisho wadau hao wameishukuru Serikali na kuiomba kuongea na mabenki ambayo walikopa fedha kuwapa muda kidogo wa kuweza kujipanga kurejesha mikopo hiyo, Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo ametoa rai kwa wafanyabiasha hao kuongeza ulinzi lakini pia katika vituo vya mafuta pasiwe na biashara tena zingine ili kujihakikishia usalama zaidi.

Matangazo

  • DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 July 17, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA WA DARASA LA SABA MEI, 2025 July 18, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MWANAFUNZI ALIYEADHIBIWA-MAKUMBUSHO SEKONDARI September 23, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MWANAFUNZI ALIYEADHIBIWA-MAKUMBUSHO SEKONDARI September 23, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Akutana na Wadau wa Nishati ya Mafuta Dar

    November 07, 2025
  • RC Chalamila Atangaza Kurejea kwa Huduma Mbalimbali Dar

    November 05, 2025
  • RC Chalamila"Jotokezeni kwa Wingi Kupiga Kura Oktoba 29,2025, Dar ni Salama Sana"

    October 27, 2025
  • Dkt Samia Suluhu Hassan Kufanya Mikutano ya Kampeni Siku 3 Kuanzia Oktoba 21,2025

    October 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa