Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 21,2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Meya wa Jiji la Dallas nchini Marekani Mhe Eric Johnson akiwa ameambatana na ujumbe kutoka Jiji hilo ofisini kwake Ilala Boma Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao mambo mbalimbali yamejadiliwa ikiwemo kukuza mahususiano ya kibiashara, uwekezaji, na utalii kwa lengo kukuza uchumi wa pande zote mbili
Aidha ujio wa Meya wa Jiji la Dallas nchini Marekani ni ishara ya kuimarika kwa Diplomasia ya Kimataifa kati ya Tanzania na Marekani vilevile uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kukuza mahususiano ya kidiplomasia ndani na nje ya nchi
RC Chalamila akimkabidhi zawadi Meya wa Jiji la Dallas Mhe Eric Johnson alipomtembelea ofisini kwake Ilala Boma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa