• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Akagua Miradi ya Maendeleo na Kuzungumza na Wananchi

Posted on: February 22nd, 2024

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Februari 22, 2024 amehitimisha ziara yake Wilaya ya Kinondoni katika jimbo la Kawe kwa kukagua miradi na kuzungumza na Wananchi eneo la Mabwepande-Kinondo


RC Chalamila katika ziara hiyo amefungua nyumba ya Mwalimu(2 in 1) Katika shule ya Sekondari Godwin Gondwe Kunduchi ambapo alipata wasaa wa kuzungumza na wanafunzi pamoja walimu wa Shule hiyo huku akiwataka wanafunzi kusoma kwa bidii kutokana na uwekezaji mkubwa ambao Rais Dkt Samia amefanya na anaendelea kufanya.

Aidha RC Chalamila pia amekagua mradi wa Hospital ya Wilaya ya Kinondoni- Mabwepande ambayo imejengwa kisasa inatoa huduma mbalimbali za Afya, vifaa tiba vya kisasa kwa sasa imeanza kutoa huduma za kuhifadhi maiti ambapo kwa siku inaweza kuhifadhi maiti 12 kwa wakati mmoja.

Vilevile RC Chalamila ametembelea kiwanda cha Smart Industry Limited kujionea uzalishaji na Changamoto ambapo amesema Serikali ya Mkoa inavutia uwekezaji wa ndani na nje kwa masilahi mapana ya wakazi wa Mkoa na Taifa kwa Ujumla

Sambamba na hilo RC Chalamila amefanya mkutano wa hadhara na Wananchi wa Mabwepande-Kinondo ambapo amesikiliza kero mbalimbali ikiwemo kero za urasimishaji wa Ardhi, migogoro ya Ardhi, Barabara, ufinyu wa huduma ya usafiri wa umma  na nyingine nyingi  ambapo kero nyingi zilizoibuliwa zilipatiwa majawabu papo hapo kwa kuwa katika ziara hiyo Mhe RC Chalamila ameambatana na wataalam wa sekta zote.

Pia RC Chalamila wakati wa mkutano huo wa hadhara amekabidhi vitendea kazi (Pikipiki) kwa jeshi la polisi na Bajaji kwa maafisa biashara wa Manispaa kwa ajili ya kukusanya Mapato.

Ifahamike kuwa Mhe Albert Chalamila ameridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo la Kawe-Kinondoni na amewataka viongozi wa Wilaya hiyo kuendelea kusikiliza na kutatua kero za wananchi, ambapo Februari 23, 2024 anatarajia kuendelea na ziara yake Wilaya ya Ubungo

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa