• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Akabidhi Pikipiki 30 Jeshi la Polisi- DSM

Posted on: October 7th, 2024

Katika hatua ya kuimarisha ulinzi na usalama katika Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila Leo Oktoba 7,2024 amekabidhi pikipiki 30 kwa vyombo vya dola katika hafla iliyofanyika eneo la Police Mess na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya,Makatibu Tawala wa Wilaya,Viongozi mbalimbali wa Dola na Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali za Serikali.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Chalamila amewashukuru sana vyombo vya dola kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kulinda usalama wa wananchi, hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa ambapo amesisitiza Polisi kuendelea kusimamia usalama ili Tanzania hususani Dar es salaam kuendelea kuwa kisiwa cha Amani.

Aidha, RC Chalamila amewataka wananchi wote kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura tarehe 11 Oktoba 2024 ili waweze kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaoanza tarehe 27 Novemba 2024. Amesema kuwa ushiriki wa wananchi katika uchaguzi ni muhimu sana kwa kuimarisha demokrasia na maendeleo ya Nchi.

Vilevile RC Chalamila amewashukuru sana Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali kama vile TPA, TCRA na DAWASA kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha katika kufanikisha ugawaji wa pikipiki hizo ambapo amesema kuwa ushirikiano huu ni muhimu sana kwa ajiri ya maendeleo katika Mkoa.

Kwa upande wao, Viongozi wa vyombo vya dola wameshukuru na kuahidi kutumia vizuri pikipiki hizo katika kuongeza ufanisi kwenye majukumu yao ikiwemo kuimarisha ulinzi na usalama Mkoani humo.

Naye Meya wa Halmashauri ya Kinondoni Bw. Songoro Mnyonge amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa pamoja na kuwa na ushirikiano wa namna ya kuweza kupata maendeleo na utulivu.

Mwisho Mhe.Chalamila ameahidi kuendelea kutoa pikipiki hizo na magari kwa siku za usoni pia amewakumbusha maaskari wote umuhimu wa kuwekeza sehemu ya fedha wanazopata ili kuweza kujikwamua kiuchumi, amesema kuwekeza ni njia moja nzuri ya kuhakikisha kuwa maisha yao yanakuwa bora zaidi.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Temeke Yang'ara Mwenge wa Uhuru 2025

    June 02, 2025
  • RC Chalamila: Miradi 36 yenye Thamani ya Tsh 79,255,160,719.44 Kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Dar

    June 01, 2025
  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa