• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Agawa Mitungi ya Nishati ya Puma Energy

Posted on: October 11th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila Leo Oktoba 11,2024 amegawa mitungi ya gesi kutoka 'PUMA ENERGY' iliyofanyika katika Viwanja vya Biafra-Kinondoni, tukio ambalo lilihudhuriwa na Wakuu wa Wilaya,Wakuu wa Taasisi, Wakurugenzi pamoja na makundi mbalimbali ya kina mama lishe na baba lishe.

Kufanyika kwa tukio hilo ni mwendelezo wa kuunga mkono kampeni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu umuhimu wa kutumia Nishati Safi ambapo zaidi ya mitungi 800 ya gesi imetolewa kwa makundi mbalimbali ili waweze kuwa mabalozi wa kuhamasisha matumizi endelevu ya Nishati safi.

Aidha Mhe. Chalamila ameeleza umuhimu wa matumizi ya Nishati safi kama njia ya kuokoa kizazi cha kina mama kuondokana na matumizi ya Nishati chafu ambayo hudhoofisha Afya ya kina mama kupitia magonjwa mbalimbali kama vile ugonjwa wa mapafu,hivyo kwa kutumia Nishati safi itaweza kumsaidia mama kuepukana na athari hizo.

Vilevile RC Chalamila ametangaza kuwepo kwa Tamasha la Mapishi kwa kutumia Nishati safi siku ya Jumamosi, Novemba 2,2024 katika Viwanja vya Biafra-Kinondoni na kutoa maagizo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bi. Halima Bulembo akisaidiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kutafuta fedha isiyopungua Mil.100 kwa ajili ya watu 2000 watakaowahi kufika katika Tamasha hilo.

Pia RC Chalamila amewaagiza Wakuu wa Wilaya ya Temeke,Ilala,Kinondoni na Ubungo kushirikiana kuratibu siku ya Tamasha la Mapishi ambalo litaambatana na  'Jogging club' watakaoanzia Magomeni mpka Biafra, kuandaa Ng'ombe watakaochinjwa na kuliwa siku hiyo, pamoja na kukaribisha makampuni ya vinywaji kama TBL,SBL,KONYAGI, PEPSI na COCA COLA kuja kuunga mkono na kujumuika katika Tamasha hilo.

Mwisho, Mkurugenzi Mtendaji wa PUMA GAS Bi.Fatma Abdallah ameelezea matokeo ya kutumia Nishati safi kama njia rahisi na salama ya kupikia na kulinda Afya ya Mama  na makazi yake kwa ujumla.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Temeke Yang'ara Mwenge wa Uhuru 2025

    June 02, 2025
  • RC Chalamila: Miradi 36 yenye Thamani ya Tsh 79,255,160,719.44 Kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Dar

    June 01, 2025
  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa