• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Afungua Semina ya TPDC kwa Viongozi wa Dini na Serikali

Posted on: August 15th, 2024

 

-Atoa rai kwa washiriki wote kuwa mabalozi na walimu wazuri kuhusu ulinzi wa miundombinu ya TPDC

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Agosti 15, 2024 amefungua semina muhimu kwa viongozi wa Dini na Serikali wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao wamepitiwa na miundombinu ya gesi asilia katika ukumbi wa mikutano wa JNICC, Semina ambayo imeandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)

RC Chalamila akifungua Semina hiyo amepongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa  kufanikisha semina hiyo muhimu kwa Viongozi wa Serikali na Viongozi wa Dini wa  Jijini Dar es salaam ambao wamepitiwa na miundombinu ya gesi asilia kwenye Wilaya za Ubungo, Kinondoni, Ilala na Temeke, ambapo amesema hilo linadhihirisha ushirikiano na uhusiano mzuri wa kidugu, uliopo kati ya TPDC na maeneo yaliyopitiwa na bomba la gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es salaam.

Aidha RC Chalamila amesema kuwa Serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa kielelezo katika bara letu la Afrika na Dunia kiujumla katika mapambano ya kupiga vita matumizi ya nishati chafu ya kupikia, TPDC kupitia gesi asilia ni mdau mkubwa katika kuhakikisha hili

Vilevile amewapongeza Viongozi wote walioshiriki warsha hiyo muhimu ambayo itawajengea uwezo katika kuisemea vyema Serikali kwenye sekta ya mafuta na gesi

Sanjari na hilo RC Chalamila amesema Serikali imeweka mikakati mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wake  wanatumia nishati safi ya kupikia ambapo tunategemea kwamba ndani ya miaka 10 kuanzia 2024-2034 80% ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.Hivyo kupitia TPDC naamini Wananchi wengi watanufaika na matumizi ya gesi asilia kwenye magari, majumbani, viwandani na kwenye umeme.

Mwisho Mhe Mkuu wa Mkoa amewatakia wote kila la heri katika utekelezaji wa majukumu yao, na kufungua rasmi semina hiyo. 


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa