-Asema wasanii wanamchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa
-Awataka kupitia kazi zao za sanaa kufikisha ujumbe wa matumizi ya matokeo ya Sensa ya mwaka 2022 kwa jamii
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Juni 12,2024 amefungua mafunzo ya matumizi ya matokeo ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa wasanii wa Mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Kiramuu, Mbezi-Beach
RC Chalamila akifungua mafunzo hayo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanazania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyowekeza na kujali wasanii hapa nchini ambapo ameweza kuanzisha mfuko maalum wa wasanii
Vilevile RC Chalamila ametoa rai kwa wasanii hao kupitia kazi zao za sanaa kuweka jumbe za matumizi ya matokeo ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ili wananchi waliowengi wapate kuelewa matumizi ya matokeo ya Sensa baada ya mafanikio makubwa ya takwimu za Sensa yaliyopatikana baada ya kukamilisha zoezi la kuhesabu
Sanjari na hilo RC Chalamila amesema wasanii ni kundi muhimu ni viziri Kabla hatujadhibiti kazi ya msanii kufanyike mjadala kujua historia yake na mambo mengine hatimaye ajengewe uwezo zaidi “ Wasanii wanaweza kuwasilisha kwa watu wengi ujumbe mgumu kwa wepesi na watu wakauelewa” Alisema RC Chalamila
Mwisho mafunzo hayo kwa wasanii yameratibiwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu ambapo kundi la wasanii kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni kundi la kwanza kupatiwa mafunzo hayo hivyo kutokana na nguvu kubwa ya wasanii katika jamii ni ukweli pasina Shaka ujumbe wa matumizi ya matokeo ya Sensa unakwenda kuifikia idadi kubwa ya watu nchi nzima
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa