• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Afanya Ziara ya Kimkakati Jimbo la Kibamba Wilaya ya Ubungo

Posted on: August 13th, 2024

 

-Akagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kufanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa mpira Makuti Kata ya Msigani.

-Amshukuru Rais Dkt Samia kwa kutekeleza miradi Lukuki katika Wilaya hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila leo Agosti 13,2024 amefanya ziara ya kukagua miradi  mbalimbali ya maendeleo, kisha kufanya Mkutano wa hadhara kwa lengo la kuwapatia Wananchi fursa ya kutoa kero zao na kuzipatia majawabu papo hapo.

RC Chalamila akiwa katika Jimbo la kibamba wilaya ya Ubungo amekagua ujenzi wa mradi wa nyumba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ambapo ametoa maelekezo kwa mkandarasi wa ujenzi huo kukamilisha ujenzi haraka ili mradi huo uanze kutumika mara moja,

Vilevile RC Chalamila alitembelea barabara ya Matosa - Temboni yenye urefu wa kilomita 3 pamoja na mradi wa maji(DAWASA) katika kata ya Kwembe.

Aidha Mhe. Chalamila amepongeza Wilaya ya Ubungo hususani Jimbo la Kibamba kwa jitihada wanazofanya katika usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ambapo amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa nyingi ambazo zimefanikisha utekelezaji wa miradi mingi katika Jimbo hilo tena miradi yenye masilahi mapana kwa wananchi.

Sanjari na hilo RC Chalamila ameonesha kutokuridhishwa na mradi wa maji katika kata ya Kwembe na kuwataka mamlaka husika kuweka mikakati inayoeleweka ya kutatua kero za wananchi walioonekana kulalamikia ukosefu wa maji katika maeneo hayo hivyo ameagiza tatizo hilo lishughulikiwe ndani ya muda mfupi.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Hassan Bomboko amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kufanya ziara ambapo amemhakikishia kutekeleza maagizo na maelekezo yake mapema iwezekanavyo ili kuleta ustawi wa wana kibamba

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila: Miradi 36 yenye Thamani ya Tsh 79,255,160,719.44 Kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Dar

    June 01, 2025
  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa