• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Aelekeza Kuundwa Kamati ya Kutatua Mgogoro wa Ardhi Sahara-Mabibo

Posted on: July 19th, 2025

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila ameelekeza kuundwa kwa kamati maalum itakayofanyakazi kwa muda wa siku tatu kuanzia julai 21 hadi 23 kushughulikia mgogoro umiliki wa uwanja wa Sahara kati ya wananchi wa mtaa wa mabibo na Saccos ya wafanyakazi wa shirika la posta na simu ambapo pande zote zinadai kuwa ni wamiliki halali

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sahara uliopo Mabibo Wilaya ya Ubungo RC Chalamila amesema lengo la kamati hiyo ni kijiridhisha uhalali wa vielelezo na maelezo yaliyotolewa na pande zote mbili kabla ya kutoa uamuzi hivyo anahitaji kamati hiyo kujumuisha wananchi,wanaushirika wa Sacoss ya shirika la posta na simu pamoja na wataalamu kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

Aidha RC Chalamila amehimiza wananchi kuwa na utamaduni wa kuwa na nyaraka za umiliki wa ardhi yaani hati badala ya maelezo ya mdomo kwani kukosekana kwa nyaraka kunaweza kupelekea mtu kupoteza haki yake.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila ametumia mkutano huo wa hadhara kuwataka wananchi kuendelea kudumisha amani utulivu na mshikamano wa nchi wakati taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu licha ya tofauti za kisiasa kwani amani ni muhimu kwa maendeleo ya nchi na makuzi ya shughuli za kiuchumi

Awali kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Wakili Albert Msando ametoa taarifa ya mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 30 tokea mwaka 1994 ambapo amesema kwa mujibu wa nyaraka zilizopo zinaonesha eneo hilo linamilikiwa na Sacoss ya wafanyakazi ya shirika la posta na simu.

Vilevile Kabla ya uamuzi huo wa kuunda kamati Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amepata nafasi ya kusikiliza maelezo ya pande hizo mbili za mgogoro ambapo wananchi wamedai eneo hilo ni kwa ajili ya michezo na wanahitaji litumike pia kujenga kituo cha afya huku mwakilishi wa saccos ya wafanyakazi wa shirika la posta na simu akieleza kuwa eneo hilo walilipata kutoka kwa iliyokuwa Sacoss ya Akilimali

Matangazo

  • DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 July 17, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA WA DARASA LA SABA MEI, 2025 July 18, 2025
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Tanzania Mwenyeji Ufunguzi wa "African Nations Championship" CHAN

    July 21, 2025
  • RC Chalamila Akutana na Meya wa Jiji la Dallas-Marekani

    July 21, 2025
  • RC Chalamila Aelekeza Kuundwa Kamati ya Kutatua Mgogoro wa Ardhi Sahara-Mabibo

    July 19, 2025
  • RC Chalamila Ataka Wataalam Kuja na Suluhu ya Msongamano wa Magari Dar

    July 11, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa