• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Aagiza TAKUKURU Kuchunguza Mgogoro wa Ardhi Kigamboni

Posted on: August 18th, 2023

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Agosti 18, 2023 ameiagiza  Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Kigamboni kuchunguza mgogoro wa Ardhi Mtaa wa Muhimbili na Kichangani- Wilaya hiyo

RC Chalamila amekitaka chombo hicho kuanza kuchunguza uhalali wa kiasi cha milioni 800 iliyolipwa na makazi kwa Ndg Julius Maganga, pili kuchunguza kodi ya Serikali kama ililipwa na wapi, vilevile kutumia hadidu za rejea za ripoti ya awali ambazo ziko tayari kuanza kuchunguza taarifa hizo " TAKUKURU tumieni mamlaka zenu zote" Alisema Mhe Chalamila

Aidha RC Chalamila ameagiza Ofisi ya Naibu Kamishna wa Ardhi Mkoa huo kusitisha mara moja utoaji wa Hati za Ardhi katika eneo hilo kuanzia leo Agosti 18, 2023, Hata hivyo amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni kuanza kufanya uhakiki wa wamiliki wote wa Ardhi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo ili kukabiliana na utapeli wa Ardhi katika Wilaya hiyo.

Sambamba na hilo RC Chalamila amewataka Wakuu wa Wilaya zote 5 katika Mkoa huo kuanzisha Clinic za Ardhi katika maeneo yao ili kutatua migogoro mbalimbali ya Ardhi kama anavyofanya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Halima Bulembo

Vilevile Naibu Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Shukrani Kyando akitoa ufafanuzi wa kitaalam amesema kutokana na taarifa zilizoko ni wazi taratibu Stahiki hazikufuatwa za umiliki wa eneo hilo, viko viashiria vya kufoji nyaraka na udanganyifu hivyo Ofisi yake iko tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo na kupokea maelekezo ya Mhe Mkuu wa Mkoa.

Mwisho Dhamira ya Serikali ni kumaliza migogoro ya Ardhi hivyo RC Chalamila ameelekeza yeyote atakayekataa kutoa ushirikiano apatiwe taarifa mara moja

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa